31.2 C
Dar es Salaam
Friday, March 29, 2024

Contact us: [email protected]

Apple Music yamtambulisha rapa Yaw Tog

Na Mwandishi Wetu

Kampuni ya Apple Music imemtangaza, Yaw Tog kutoka Ghana kama msanii mpya katika programu yake ya ukuzaji wa vipaji vya wasanii barani Afrika uitwao Africa Rising.

Yaw Tog ambaye jina lake halisi ni Thorsten Owusu Gyimah ni kijana mdogo mwenye umri wa miaka 17 lakini ni moto wa kuotea mbali, kutokana na uwezo wake wa kurap kisasa kunakopagawisha mashabiki.Akizungumza baada ya kupata shavu hilo, Yaw Tog anasema: “Nimefurahi sana kuheshimiwa kuwa msanii anayefuata wa Africa Rising.

“Ninashukuru sana kwa msaada na upendo ambao mashabiki wangu, wapenzi wa muziki wangu kote ulimwenguni na timu ya Apple Music wamenionyesha hadi sasa. Sichukulii hii kawaida na ninachoweza kuahidi ni kwamba nitaendelea kufanya kazi kwa bidii na kuipaisha nchi yangu ya Ghana kwenye ramani ya muziki duniani,” amesema.

Msanii huyo ambaye anaimba mtindo uitwao Asakaa, ulioibuka kutoka Kumasi nchini Ghana, wimbo wake wa kwanza kumtambulisha ulikuwa ni “Sore” (2020) ambao ulifuatiwa na video yake ambayo ilitazamwa na zaidi ya watu milioni 1 ulimwenguni.

Akishirikiana na O’Kenneth, City Boy, Reggie, Jay Bhad, wote wakiimba mtindo wa Asakaa ambao ni utambulisho wao wa kipekee wa maisha ya mitaani katika maeneo ya Kumasi iliyoingizwa na utamaduni wa kupigiwa debe.

Msanii huyo licha ya kuwa mchanga, ana utajiri wa lugha kwani anatumia lugha za Kiingereza, Twi (lugha ya Kwa inayozungumzwa na watu milioni kadhaa nchini Ghana) na Pidgin, wakati wa kuunganisha vitu vya Afrobeats na Hip-hop.

Apple Music’s Africa Rising ni programu ya kipekee ya ukuzaji wa wasanii na orodha ya kucheza inayokusudiwa kutambua, kuonyesha na kuinua talanta inayoibuka na kuanzisha kizazi kijacho cha superstars za Kiafrika.

Hadi sasa, wasanii walionufaika na programu hii ni pamoja na Omah Lay, Manu Worldstar, Tems, Amaarae na Ayra Starr. Wateja wa Apple Music wanaweza kufurahia muziki mzuri kupitia kwenye mifumo ya simu za iOS na Android nchini Kenya, Tanzania, Uganda, Nigeria, Afrika Kusini, Ghana, Botswana, Msumbiji, Kameruni na Zambia.

- Advertisement -

Related Articles

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Stay Connected

90,904FansLike
214,997FollowersFollow
585,000SubscribersSubscribe

Latest Articles