Kadinda kutamba na ‘Kambale’ Afrika Kusini

0
1416

martin_kadindaNA JENNIFER ULLEMBO, DAR ES SALAAM
MBUNIFU wa mavazi Tanzania, Martin Kadinda, anatarajia kuonyesha mitindo mbalimbali aliyoipa jina la ‘Kambale’ katika maonyesho maalumu yatakayojulikana kama wiki ya mavazi, nchini Afrika Kusini.
Akizungumza na MTANZANIA jana, Kadinda ambaye aliondoka jijini jana jioni kuelekea Afrika Kusini, alisema mitindo hiyo itajumuisha mavazi ya kiume na viatu vyake vya ‘Mugat’
Alisema maonyesho hayo yamepangwa kuanza kufanyika Jumatano lakini yeye atapanda jukwaani Alhamisi kuonyesha mitindo yake.
“Nina imani maonyesho haya ni hatua nzuri ya kutangaza kazi zangu na kulitangaza taifa langu la Tanzania, lazima tujivunie ubunifu wetu,” alisema Kadinda.

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here