29.2 C
Dar es Salaam
Thursday, November 28, 2024

Contact us: [email protected]

Kada CCM kizimbani kwa kuishi bila kibali

Na KULWA MZEE-DAR ES SALAAM

IDARA ya Uhamiaji imemfikisha mahakamanj kada maarufu wa wa Chama cha Mapinduzi (CCM) Mkoa wa Iringa, Michael Mlowe kwa tuhuma za kuishi nchini bila kibali na kutoa taarifa za uongo  kuhusu uraia wake.

Mlowe ambaye kwa jina maarufu ni Mayko Namlowe (44) ni raia wa Uingereza, alifikishwa  katika Mahakama ya Hakimu Mkazi Kisutu  jana na kusomewa mashtaka mbele ya Hakimu Mkazi Mwandamizi, Augustina Mmbando.

Wakili wa Serikali kutoka Idara ya Uhamiaji, Novatus Mlay alidai mshitakiwa  huyo  ni mfanyabiashara na mkazi wa Lugalo Kihesa, Iringa.

Mshitakiwa anadaiwa kwamba  Mei 31, mwaka huu  katika Makao Makuu ya Ofisi ya Uhamiaji   Wilaya ya Temeke akiwa raia wa Uingereza, aliishi nchini akiwa hana Viza wala nyaraka yoyote inayomwezesha kufanya hivyo.

Mlay alidai katika shtaka la pili, Mlowe anadaiwa kutengeneza hati bandia,  inadaiwa  Mei 31, mwaka huu katika ofisi hizo za uhamiaji akiwa raia wa Uingereza alitoa taarifa ya uongo inayohusiana na uraia wake.

Kwa kufanya hivyo mshtakiwa alijipatia kitambulisho cha taifa namba 19741219-51108-00001-24 ambacho kina jina la Michael Juma Mlowe wakati akijua alichokifanya ni kosa.

Mshtakiwa alikana kutenda makosa hayo, upelelezi haujakamilika na Jamhuri haikuwa na pingamizi kwa mshtakiwa kupata dhamana.

Wakili wa utetezi, Kashindye Thabiti aliiomba mahakma impe dhamana mteja wake kwa vile  shtaka linalomkabili lina dhamana.

Hakimu Mmbando alikubali kumpa dhamana mshtakiwa kwa masharti ya kuwa na wadhamini wawili wa kuaminika, wenye barua na vitambulisho.

Mshtakiwa alitimiza masharti ya dhamana, yuko nje kwa dhamana hadi Novemba 1 mwaka huu kesi yake itakapotajwa tena.

- Advertisement -

Related Articles

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Stay Connected

90,904FansLike
214,997FollowersFollow
592,000SubscribersSubscribe

Latest Articles