26.7 C
Dar es Salaam
Monday, June 24, 2024

Contact us: [email protected]

Kada CCM ajipanga kumvaa Mrema Vunjo

Augustine Mrema
Mbunge wa Vunjo (TLP), Augustine Mrema

Na Mwandishi Wetu, Dar es Salaam

NAIBU Kamanda wa Umoja wa Vijana wa Chama Cha Mapinduzi (UVCCM) Wilaya ya Moshi Vijijini, mkoani Kilimanjaro, Innocent Melleck, amesema wakati ukifika anatarajia kugombea ubunge katika Jimbo la Vunjo, mkoani Kilimanjaro.

Alisema umefika wakati kwa vijana kuhakikisha wanagombea na kuchaguliwa katika nafasi za uongozi wa kisiasa, ili kuleta mabadiliko chanya ya kiuchumi.

Akizungumza na waandishi wa habari mwishoni mwa wiki iliyopita, Melleck alisema mwaka ujao ni mwaka wa vijana na kwamba lazima wajitokeze na kushiriki kikamilifu na kugombea nafasi katika Uchaguzi Mkuu, ukiwamo Ubunge, udiwani na hata urais.

Alisema kwa upande wake, amejiandaa vya kutosha ili kuhakikisha anagombea ubunge katika Jimbo la Vunjo, ambalo kwa sasa linaongozwa na Augustino Mrema (TLP).

“Nawakumbusha vijana wote ifikapo mwakani lazima wawe na ajenda mahususi za kuwaambia wananchi ili kuwashawishi wawachague na baada ya kupata ridhaa hiyo watekeleze watakachokuwa wameahidi.

“Baadhi ya majimbo yamedumaa kimaendelea, likiwamo la Vunjo, kutokana na viongozi wake kutokuwa na mawazo ya kutaka kuleta mabadiliko yanayokwenda na wakati.

Aliongeza kuwa ajenda yake katika Uchaguzi Mkuu ujao ni kuhakikisha anawaunganisha vijana wa Vunjo na wananchi wengine kulipa kipaumbele zao la ndizi ambalo alisema kwa sasa halitoi matokeo chanya kwa wakulima.

Melleck, anayejulikana na wananchi wa Vunjo kama ‘Tumaini jipya’, alisema uwezo wa kulifanya zao la ndizi liwe zao mbadala wa kahawa anao na kwamba wananchi wanahitaji kushirikishwa.

Aliwataka wana CCM kutorudia makosa, ikiwamo kuwapa jimbo wanasiasa kutokana na mazoea, bali waangalie viongozi ambao wamedhamiria kuleta mabadiliko chanya.

- Advertisement -

Related Articles

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Stay Connected

90,904FansLike
214,997FollowersFollow
588,000SubscribersSubscribe

Latest Articles