25.2 C
Dar es Salaam
Wednesday, April 24, 2024

Contact us: [email protected]

Kabila atangaza kutokuwania Urais tena

4bhk9e73c47c201jzm_800c450
Rais Joseph Kabila

Rais wa Jamhuri ya Demokrasi ya Congo Joseph Kabila, amelihutubia Bunge la Taifa leo na kuwahkikishia wananchi kuwa hatogombea tena Urais katika uchaguzi mkuu ujao.

Rai Kabila amesema anaiheshimu katiba ya nchi yake na kwamba ataifuata huku akisisitiza kuwepo kwa amani na utulivu.

“Jahmuri ya Kidemorisia ya Congo ni nchi inayoongozwa na katiba hatujakiuka katiba na tutaendelea kuiheshimu. Kwa mda huu kilicho muhimu ni kuangalia maisha ya wakongo,” alisema Kabila.

Hata hivyo, jana waziri mkuu Augustina Matata Ponyoa alijiuzulu kutoa nafasi wadhifa huo kuchukuliwa na upinzani kwenye utawala wa mpito.

Hatua hii ni ya kutuliza vurugu za kisiasa nchini humo baada ya vyama vikuu vya kisiasa kususia mazungumzo ya kitaifa.

Awali Kamisheni ya Uchaguzi katika Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo iliahirisha uchaguzi wa rais uliokuwa umepangwa kufanyika mwaka huu hadi mwezi Julai mwakani.

Pia, Mahakama ya juu ya Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo ilitangaza kuwa iwapo serikali ya Rais Joseph Kabila haitaweza kuandaa uchaguzi wa rais katika wakati ulioainishwa basi kiongozi huyo anaweza kubakia madarakani. 

Kabila alishika hatamu za kuiongoza Congo mwaka 2001 baada ya mauaji ya baba yake, Laurent Kabila, na kisha akashinda uchaguzi wa rais uliofanyika mwaka 2006. 

- Advertisement -

Related Articles

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Stay Connected

90,904FansLike
214,997FollowersFollow
586,000SubscribersSubscribe

Latest Articles