Na Mwandishi wetu
Jeshi la Ulinzi la Wananchi wa Tanzania (JWTZ) kwa kushirikiana na Jeshi la Marekani wanatarajia kufanya mafunzo maalumu kukabiliana na vitendo vya uhalifu ikiwamo ugaidi.
Hafla ya kufungua mafunzo hayo, umefanyika leo Julai 28,2021 katika Kituo cha Ulinzi wa Amani Kunduchi, Dar es Salaam.
Akizungumza katika hafla hiyo, Mkuu wa Kamandi ya Afrika wa Jeshi la Marekani, Jenerali Stephen Townsend, amesema Tanzania na Marekani zimekua na ushirikiano katika mambo mbalimbali hivyo ni sehemu sahihi katika mafunzo hayo maalumu.
Kwa upande wake Mnadhimu Mkuu wa JWTZ, Luteni Jenerali Yakoub Mohamed, amesema jeshi la Marekani limekua likishirikiana vyema na Jeshi la Wananchi wa Tanzania katika mafunzo mbalimbali.
Amesema mafunzo hayo maalumu ya yatakuwa ya mwezi mmoja lengo likiwa kukomesha vitendo vya uhalifu ikiwemo, ugaidi na vitendo vingine kama hivyo ambavyo vimekua vikitokea katika Mataifa mbalimbali.