30.2 C
Dar es Salaam
Thursday, May 23, 2024

Contact us: [email protected]

Jumba la Nyerere lazinduliwa Ethiopia

Jengo la Umoja wa Afrika la Julius Nyerere la Amani na Usalama
Jengo la Umoja wa Afrika la Julius Nyerere la Amani na Usalama

ADDIS ABABA, ETHIOPIA

KANSELA wa Ujerumani, Angela Merkel amezindua jumba jipya la Makao Makuu ya Umoja wa Afrika (AU) ambalo limepewa jina la Rais wa kwanza wa Tanzania, Mwalimu Julius Nyerere.

Jumba hilo, ambalo jina lake kamili ni Jumba la Amani na Usalama la Julius Nyerere limejengwa kwa ufadhili wa Ujerumani.

Litakuwa makao ya Idara ya Amani na Usalama ya AU na litatumiwa pia na maafisa wa kutoa tahadhari ya mapema kuhusu mizozo barani humu pamoja na kuratibu juhudi za kulinda amani za AU.

Ujenzi wa jumba hilo, ambalo ukubwa wake wa sakafu ni mita 13,500 mraba na linaweza kutumiwa na wafanyakazi 360, uligharimu euro milioni 27.

Jumba hilo lenye ofisi za kufanyia kazi, vyumba vya mikutano kwa ajili ya Baraza la Amani na Usalama, chumba cha kuratibia shughuli, maktaba na vyumba vya shughuli nyinginezo.

Mwalimu Nyerere, ambaye alikuwa rais wa Tanzania hadi mwaka 1985, alikuwa mmoja wa viongozi waanzilishi wa Muungano wa Nchi Huru za Afrika (OAU) ambao  sasa unajulikana kama AU.

Aliongoza harakati za kuendeleza Bara la Afrika na kusaidia mataifa ambayo hayakuwa yamepata uhuru kujipatia uhuru wake.

Mwalimu Nyerere alipigania sana kumalizika kwa utawala wa mabavu wa ubaguzi wa rangi wa wazungu wachache katika nchi za Rhodesia (sasa Zimbabwe), Afrika Kusini, na Taifa la Kusini Magharibi mwa Afrika (sasa Namibia).

- Advertisement -

Related Articles

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Stay Connected

90,904FansLike
214,997FollowersFollow
587,000SubscribersSubscribe

Latest Articles