29.2 C
Dar es Salaam
Sunday, June 23, 2024

Contact us: [email protected]

Juma Nature kujivunia miaka 16 ya mafanikio yake

JUMANA HADIA KHAMIS
MSANII mwenye jina kubwa katika muziki wa Bongo Fleva nchini, Juma Kassim Kiroboto ‘Juma Nature’, anatarajia kusherehekea miaka 16 ya mafanikio yake hivi karibuni.
Mafanikio hayo atayafurahia katika tamasha la Komaa Concert ambapo watashirikiana na kituo cha Redio cha EFM kinachosherehekea mwaka mmoja tangu kuanzishwa kwake.
Mkurugenzi wa mawasiliano wa kituo hicho, Dennis Sebbo, alisema tamasha hilo litafanyika katika Manispaa ya Temeke ikiwa ni heshima ya msanii huyo kwa kuzaliwa huko na ni wilaya ambayo kitio hicho kilianzishwa kwa mara ya kwanza.
Nature alisema ataadhimisha kwa kutembelea wagonjwa katika Hospitali ya Temeke ambapo atatoa zawadi mbalimbali kwa wagonjwa kisha jioni yake ataendeleza onyesho kabambe.
“Miaka 16 ni mingi katika sanaa ukizingatia enzi hizo tunaanza kazi katika sanaa tulikuwa tunatembea kwa miguu kutoka Kurasini hadi kwa Master J, Masaki kwa ajili ya kurekodi na wakati mwingine haupati nafasi hivyo tunatakiwa tumshukuru Mungu kwa hali ilivyo sasa,” alisema Nature.

- Advertisement -

Related Articles

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Stay Connected

90,904FansLike
214,997FollowersFollow
588,000SubscribersSubscribe

Latest Articles