26.2 C
Dar es Salaam
Sunday, November 17, 2024

Contact us: [email protected]

JPM: Marufuku kuuza sare za jeshi uraiani

Rais Dk. John Magufuli
Rais Dk. John Magufuli

Na Mwandishi Wetu, Dar es Salaam

Amiri Jeshi Mkuu  Rais Dk. John Magufuli, amepiga marufuku uuza uuzwaji wa sare za majeshi nchini na watu binafsi na kutaka wale wote wanaouza wazikabidhi kwa majeshi husika mara moja.

Taarifa iliyotolea kwa vyombo vya habari Dar es Salaam jana na Naibu Mkurugenzi wa Mawasiliano Ikulu, Jaffar Haniu ilisema Rais Dk. Magufuli alifia uamuzi huo baada ya kufanya ziara ya kushtukiza katika Gereza la Ukonga,Dar es Salaam.

Taarifa hiyo, ilisema Rais Dk. Magufuli amepiga marufuku hiyo kutokana na maelezo ya baadhi ya askari wa Jeshi la Magereza kuwa wamekuwa wakinunua sare za jeshi hilo kutoka kwa watu binafsi kinyume na taratibu za majeshi.

Kutokana na hali hiyo, Rais Dk. Magufuli ameviagiza vyombo vya ulinzi na usalama kuwachukulia hatua mara moja wale wote watakaobainika kuuza sare hizo.

”Haiwezekani sare za majeshi yetu kuuzwa na watu binafsi hili haliwezekani kamwe, labda baada ya kumaliza muda wangu,” alisema Rais Dk. Magufuli”

Pia amepiga marufuku majeshi yote  kuingia ubia na watu binafsi kupangisha ama kuuza maeneo yao kwa ajili ya kufanya biashara na kutaka maeneo ya majeshi yabaki katika jeshi husika.

Katika hatua nyingine, Rais Dk. Magufuli ametoa Sh bilioni 10 kwa Jeshi la Magereza kwa ajili ya kujenga nyumba mpya zitakazotumika kwa ajili ya makazi ya askari wake katika Gereza la Ukonga.

Hatua hiyo inatokana na kilio cha askari Magereza, kuwa wengi wao wamekuwa wakiishi uraiani kitu ambacho ni tofauti na taratibu za majeshi  hata kuzorotesha utendaji kazi wao wa kila siku.

Taraifa hiyo, iliongeza kuwa ameagiza Jeshi la Magereza kuhakikisha wafungwa wanatumika ipasavyo katika uzalishaji mali,badala ya mfumo wa sasa ambapo baadhi wamekuwa  wakitutumia rasilimali za serikali bila kuzifanyia kazi.

Aliwahakikishia  maofisa na askari wa  jeshi hilo kuwa Serikali itaendelea kuboresha maslahi yao na vitendea kazi kama inavyofanya kwa majeshi mengine.

- Advertisement -

Related Articles

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Stay Connected

90,904FansLike
214,997FollowersFollow
591,000SubscribersSubscribe

Latest Articles