29.2 C
Dar es Salaam
Friday, November 15, 2024

Contact us: [email protected]

JPM KUADHIMISHA MAPINDUZI YA ZANZIBAR AKIWA SHINYANGA

magu
Rais Dk. John Magufuli akiwa amekaa na wananchi katika kibanda cha kushona na kung’arisha viatu kilichopo Stendi ya zamani Chato mkoani Geita. Kibanda hicho ndicho alikuwa aking’arisha viatu na kubadilishana mawazo na wananchi kabla hajawa Rais

 

Na KADAMA MALUNDE – SHINYANGA

RAIS Dk. John Magufuli, anatarajia kuadhimisha siku ya Mapinduzi ya Zanzibar na katika uwanja wa CCM Kambarage mkoani  Shinyanga.

Akizungumza na waandishi wa  habari jana, Mkuu wa Mkoa wa Shinyanga, Zainab Telack, alisema Rais Dk. Magufuli atawasili mkoani kesho kwa ajili ya kuadhimisha miaka 53 ya Mapinduzi ya Zanzibar kwa kuzungumza na wakazi wa Shinyanga katika uwanja wa CCM Kambarage.

“Tutakuwa na ugeni wa kiongozi wetu ambaye ataadhimisha siku ya Mapinduzi ya Zanzibar mkoani Shinyanga, tunawaomba wananchi wajitokeze kwa wingi kuja kumpokea Rais wetu,” alisema Telack.

Katika hatua nyingine, Telack alisema mkoa wa huo hauna tatizo la njaa kwani bado una  chakula  kingi ingawa kuna baadhi ya kata katika wilaya ya Kishapu ambazo zina upungufu wa chakula na tayari wameelekeza wafanya biashara kupeleka chakula katika maeneo hayo.

“Hali ya  chakula mkoa wetu ni  nzuri Shinyanga ni miongoni   mwa  mikoa yenye chakula cha kutosha, tuna tatizo kidogo Wilaya ya Kishapu katika kata ambazo hazikupata mvua na tayari tumeelekeza wafanyabiashara wanaendelea kupeleka chakula kwenye masoko ili wananchi waweze kujinunulia chakula.

“Hatujasema  tumezidiwa sana kwa sababu  tangu mwaka jana tulikuwa na ziada ya chakula katika mkoa wetu na bado tunayo kwa hiyo hatuwezi kulia sana,” alisema Telack.

- Advertisement -

Related Articles

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Stay Connected

90,904FansLike
214,997FollowersFollow
591,000SubscribersSubscribe

Latest Articles