31.8 C
Dar es Salaam
Thursday, December 12, 2024

Contact us: [email protected]

LOWASSA, SUMAYE KUTIKISA KANDA YA ZIWA

sssss
Na MWANDISHI WETU – DAR ES SALAAM

MAWAZIRI wakuu wa zamani na wajumbe wa Kamati Kuu ya Chama cha Demokrasia na Maendeleo (Chadema), Edward Lowassa na Frederick Sumaye, watafanya ziara katika mikoa ya Kanda ya Ziwa Viktoria na Serengeti.

Taarifa iliyotolewa jana na Mkuu wa Kitengo cha Habari na Mawasiliano wa Chadema, Tumaini Makene, ilisema  ziara hiyo ina lengo la kukiimarisha chama katika ngazi za chini kupitia mikutano ya ndani.

Mbali na vikao vya ndani, Sumaye na Lowassa wanatarajiwa kuhutubia mikutano ya hadhara katika baadhi ya kata ambazo zinarudia uchaguzi kwa nafasi za udiwani katika kanda hizo kadiri ya ratiba ilivyopangwa.

“Vikao vya ndani vitaanza  rasmi Januari 11 katika majimbo mbalimbali ya mikoa sita, kwenye kanda mbili za kichama za Viktoria na Serengeti, viongozi wakuu wakiambatana na wajumbe wa Kamati Kuu na wabunge, watakutana na viongozi wa chama katika ngazi za chini kupitia vikao vya mikutano maalumu ya majimbo,” alisema Makene.

Alisema Mwenyekiti wa chama hicho, Freeman Mbowe  na wajumbe wa Kamati Kuu, wataongoza timu mbalimbali zitakazofika kwenye majimbo yote ya kanda hizo hadi Januari 20.

Viongozi wakuu wengine watakaongoza timu mbalimbali ni pamoja na Makamu Mwenyekiti (Tanganyika), Profesa Abdallah Safari na Makamu Mwenyekiti (Zanzibar), Said Issa Mohamed.

Wengine ni Katibu Mkuu, Dk. Vincent Mashinji, Naibu Katibu Mkuu (Tanganyika), John Mnyika na Naibu Katibu Mkuu (Zanzibar), Salum Mwalim Juma.

Taarifa hiyo ya Chadema ilisema kuwa ziara hiyo itamalizika kwa vikao vya mabaraza ya uongozi katika kanda zote mbili kwa nyakati tofauti, kufanya uchaguzi wa kupata viongozi wa kanda hizo katika nafasi za mwenyekiti, makamu mwenyekiti na mweka hazina.

- Advertisement -

Related Articles

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Stay Connected

90,904FansLike
214,997FollowersFollow
592,000SubscribersSubscribe

Latest Articles