30.7 C
Dar es Salaam
Thursday, December 19, 2024

Contact us: [email protected]

JPM AMKINGIA KIFUA MAKONDA

ELIZABETH HOMBO Na ESTHER MBUSSI – DAR ES SALAAM

RAIS Dk. John Magufuli,  amesema hatamchukulia hatua zozote Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam, Paul Makonda na kwamba hakuna wa kumwonyesha njia ya kupita wala kumpangia kiongozi yupi anayefaa katika nafasi fulani.

Kutokana na hilo, amemtaka Makonda kuendelea kuchapa kazi na kwamba yeye hafanyii kazi maneno ya kwenye mitandao kwa sababu anajiamini.

Rais Magufuli alitoa kauli hiyo jijini Dar es Salaam jana wakati akizindua ujenzi wa barabara za mapishano ya juu (interchange) katika makutano ya Ubungo.

Alisema Watanzania wamekuwa wakijielekeza kwenye masuala ya udaku ambayo hayasaidii chochote.

“Watanzania tumejielekeza mno kwenye masuala ya udaku ambayo hayatupunguzii njaa, hayatupunguzii umasikini, matatizo ya elimu, hayatusaidii kusafiri kwenda mjini, hayatusaidii kununua nguo, hayatusaidii kununua mchicha, hayatusaidii kupata dawa za hospitali…lakini haya mambo ya umbea ndio yanachukua muda wetu mwingi.

“Mnapost  vipost vyenu mara hivi mara vile mpaka wengine mnaingilia uhuru wangu…ukiingilia ndiyo umepotea kabisa, mimi huwa sipangiwi mambo, mimi ni Rais ninayejiamini…ndiyo maana nilipoenda kuchukua fomu ya kugombea urais hakuna aliyenipangia,  nilichukua mwenyewe kwa sababu niliona ‘nafit’ (nafaa) kuwa Rais.

“Hakuna wa kunipangia nani nimuweke wapi, mimi ndiyo napanga fulani anakaa wapi, hakuna wa kunionyesha mimi njia ya kupita. Chama changu CCM ndiyo kilinionesha njia kupitia ilani.

“Kwa hiyo Makonda wewe chapa kazi achana na hayo yanayosemwa kwenye mitandao, hayana tija piga kazi tu…nadhani wamenielewa, hata mimi huwa ninaandikwa sasa nikiandikwa kwa hiyo nijiuzulu urais…kuandikwa kwangu si tija bali kuchapa kazi,”alisema Rais Magufuli.

Kutokana na hilo, Rais Magufuli aliwataka Watanzania wajielekeze katika mambo ya maendeleo na kwamba hayana chama kwa sababu kampeni zilikwisha tangu mwaka juzi.

"Ningefurahi sana huko kwenye mitandao kama tungekuwa tunajadili jinsi ya kufanya mambo ya maendeleo.

“Kampeni zilikwisha na mimi ndiyo rais…hata ulie ujigaragaraze weweee lakini Rais ni mimi John Pombe Magufuli na kwangu ni kazi tu. " alisema.

[embedyt] https://www.youtube.com/watch?v=c7F3DR2Y2P8[/embedyt]

- Advertisement -

Related Articles

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Stay Connected

90,904FansLike
214,997FollowersFollow
592,000SubscribersSubscribe

Latest Articles