27.2 C
Dar es Salaam
Wednesday, February 8, 2023

Contact us: [email protected]

‘FLYOVER’ UBUNGO KUJEGWA USIKU, MCHANA

Rais Dk John Magufuli (kulia) na Rais wa Benki ya Dunia, Jim Yong Kim, wakizindua ujenzi wa barabara za juu eneo la Ubungo Dar es Salaam jana. PICHA: SILVAN KIWALE

Na ELIZABETH HOMBO – DAR ES SALAAM

RAIS Dk. John Magufuli, amewataka wakandarasi wanaosimamia mradi wa ujenzi wa barabara za mapishano ya juu (interchange) katika makutano ya Ubungo, kufanya kazi usiku na mchana ili mradi huo ukamilike haraka.

Mkuu huyo wa nchi alitoa kauli hiyo Dar es Salaam jana, wakati akiweka jiwe la msingi katika mradi huo, huku akishirikiana na Rais wa Benki ya Dunia, Dk. Jim Yong Kim.

Awali akizungumza kabla ya kuweka jiwe hilo la msingi, Rais Magufuli alimtaka Waziri wa Ujenzi, Uchukuzi na Mawasiliano, Profesa Makame Mbarawa, kusimamia mradi huo ili uweze kukamilika kwa wakati.

“Simamieni mradi huu ukamilike haraka sioni sababu ya mradi kuchukua muda wakati kuna usiku na mchana. Nategemea mradi huu utamalizika kabla ya miezi 30 angalau miezi 20 kwa sababu hela ipo. Kwanini usubiri miezi yote hiyo wakati unaweza kukamilisha hata kwa miezi 12,”alisema Rais Magufuli.

Mradi huo ambao utagharimu zaidi ya Sh bilioni 188 ambazo ni fedha za mkopo kutoka Benki ya Dunia, Rais Magufuli alisema lengo la mradi huo ni kupunguza foleni ambayo imekuwa kero kwa wakazi wa Dar es Salaam.

“Ni jambo la kushukuru kwa Rais huyu wa Benki ya Dunia kuja Tanzania kote huko amepita Marekani, amepita Japan lakini amekuja Dar kwenye jiji la Makonda. Tunawaomba waendelee kutupatia mkopo kwa sababu tunaweza kukopesheka.

“Benki ya Dunia wao wanatukopesha kwa riba ya asilimia 0.5 wakati mabenki mengine inafika mpaka asilimia 28,”alisema.

Rais Magufuli alisema fedha hizo zinazotumika katika mradi huo ni za mkopo hivyo Watanzania walipe kodi na kwamba waulinde mradi huo.

“Wale ambao watabahatika kufanya kazi katika mradi huu msiibe vitu ambavyo vinatumika hapa, tuulinde mradi huu na tulipe kodi,”alisema.

Alisema watajenga daraja kutoka coco beach mpaka Hospitali ya Agha Khan, ambapo daraja hiyo itapita baharini.

Pia alisema Sh bilioni 38 zimetengwa kwa ajili  ya kujenga barabara za juu katika maeneo ya Tabata, Magomeni lengo likiwa ni kuboresha barabara za jiji la Dar es Salaam.

Alisema mradi mwingine uliosainiwa ni wa kuboresha huduma katika mikoa ya Arusha, Dodoma na mengine.

RAIS WA WB

Kwa upande wake Rais wa Benki ya Duania, Dk. Jim Yong Kim alisema amevutiwa na kiwango cha matarajio na dhamira aliyonayo Rais Magufuli na kwamba ndoto zake zitaongezeka pamoja na kwamba misaada rasmi ya maendeleo inapungua.

Pamoja na mambo mengine, alisema iwapo mikopo ya kibiashara haina tija au haifai, watafanya kazi ya kupunguza hatari na kushughulikia matatizo ya soko.

“Ndio kwanza nimetoka kwenye mkutano wa G20 na ni wazi kwamba nchi nyingi kubwa za wafadhili zinaangalia zaidi mambo yao wenyewe.

“Kwa uzoefu wetu njia pekee ya kufikia  ndoto hizo ni kwa kutumia fedha za umma na rasilimali za ndani kwa njia iliyo kimkamkati zaidi kadiri inavyowezekana,”alisema Dk. Kim.

- Advertisement -

Related Articles

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Stay Connected

90,904FansLike
208,871FollowersFollow
561,000SubscribersSubscribe

Latest Articles