23.2 C
Dar es Salaam
Friday, April 19, 2024

Contact us: [email protected]

JPM AFANYA UTEUZI BODI SITA

Na MWANDISHI WETU -DAR ES SALAAM

RAIS John Magufuli amefanya uteuzi wa wenyeviti wa bodi sita za taasisi za Serikali baada ya wenyeviti waliokuwapo kumaliza muda wao.

Kwa mujibu wa taarifa iliyotolewa kwa vyomboa vya habari na Katibu Mkuu Kiongozi, Balozi John Kijazi, Rais Magufuli amemteua Monica Mbega kuwa Mwenyekiti wa Bodi ya Mazao Mchanganyiko.

Pia amemteua Profesa Egid Mubofu kuwa Mwenyekiti wa Bodi ya Wakurugenzi wa Kampuni ya Mbolea Tanzania (TFC) na Profesa Abiud Kaswamila kuwa Mwenyekiti wa Bodi ya Mamlaka ya Hifadhi ya Ngorongoro.

Profesa Esther Jason naye ameteuliwa kuwa Mwenyekiti wa Bodi ya Mamlaka ya Maabara ya Mkemia Mkuu wa Serikali.

Wengine walioteuliwa ni   Dk. Kenneth Mdadila kuwa Mwenyekiti wa Bodi ya Taasisi ya Fedha ya Self Microfinance Fund Limited, Dk. Titus Kamani kuwa Mwenyekiti wa Tume ya Maendeleo ya Ushirika Tanzania.

- Advertisement -

Related Articles

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Stay Connected

90,904FansLike
214,997FollowersFollow
586,000SubscribersSubscribe

Latest Articles