27.2 C
Dar es Salaam
Tuesday, November 26, 2024

Contact us: [email protected]

Jokate azindua kampeni ‘Tokomeza Ziro Kisarawe’

Norah Damian, Dar es Salaam



Mkuu wa Wilaya ya Kisarawe, Jokate Mwegelo, amezindua kampeni ya kutokomeza sifuri na kuongeza ufaulu katika mitihani ya kidato cha nne na sita katika Wilaya ya Kisarawe.

Akizungumza leo wakati wa uzinduzi huo uliofanyika katika Shule ya Sekondari Chanzige, amesema kupitia kampeni hiyo iliyopewa jina la ‘Tokomeza Ziro Kisarawe’ tayari wanafunzi 760 wa kidato cha nne wameanza kambi maalumu ya miezi mitatu.

“Wako wanafunzi wengine ambao hutembea umbali wa kilomita 15 kuja shule hivyo, tunaamini kwa kuwaweka pamoja kutasaidia kuweza kujiandaa vizuri na mitihani yao,” amesema Jokate.

Amesema mbali ya kuwa na kambi hiyo pia wanatarajia kuboresha miundombinu katika shule zote za sekondari mpango ambao utagharimu Sh bilioni 4.1.

Amefafanua kuwa miundombinu hiyo ni ujenzi wa madarasa, matundu ya vyoo, maktaba, ofisi za walimu na ununuzi wa madawati, meza na viti. Wilaya hiyo ina shule za sekondari 22 na kati ya hizo 16 ni za serikali na sita ni za watu binafsi.

- Advertisement -

Related Articles

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Stay Connected

90,904FansLike
214,997FollowersFollow
591,000SubscribersSubscribe

Latest Articles