26.4 C
Dar es Salaam
Tuesday, November 26, 2024

Contact us: [email protected]

JKCI kupokea rasmi rufaa za wagonjwa wa moyo kutoka Zanzibar

Na Mwandishi Wetu, Zanzibar            |               


TAASISI ya Moyo Jakaya Kikwete (JKCI) kuanzia sasa itaanza rasmi kupokea rufaa za wagonjwa wa moyo kutoka Zanzibar ili kuwatibu magonjwa hayo.

Hayo yameidhinishwa mapema leo Visiwani humo baada ya Mkurugenzi Mtendaji wa JKCI, Profesa Mohamed Janabi na Katibu wa Wizara ya Afya Zanzibar, Asha Ali Abdullah kutiliana saini ya makubaliano.

“Tumesaini makubalino, lakini kabla hatujafikia hatua hii tayari wagonjwa 50 kutoka visiwani hapa wamenufaika na huduma zetu pale JKCI, hivyo sasa ni rasmi wagonjwa watapewa rufaa kuja kutibiwa pale, watanufaika wengi,” amesema.

Amesema tangu mwaka 2015 hadi sasa zaidi ya wagonjwa 200,000 wamepatiwa matibabu katika taasisi hiyo na kwamba ikiwa wagonjwa hao wangepelekwa nje ya nchi ingechukua miaka 14 kufikia idadi hiyo.

“Serikali (Tanzania Bara) kila mwaka ilikuwa inawapa rufaa kwenda nje kutibiwa takriban wagonjwa 400 na 200 kati yao walikuwa ni wa moyo, kila mmoja aligharimu kiasi cha Sh milioni 29,” amesema.

Amesema kila siku wanaona wagonjwa 300 katika kiliniki zao, wanapokea kwa rufaa wagonjwa wa moyo kutoka nchini Uganda, Kenya, Malawi, Zambia, Jamhuri ya Kidemokrasia ya Kongo na kuwatibu.

- Advertisement -

Related Articles

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Stay Connected

90,904FansLike
214,997FollowersFollow
591,000SubscribersSubscribe

Latest Articles