22.9 C
Dar es Salaam
Thursday, September 19, 2024

Contact us: [email protected]

JK Mzungu Gym kufanya tamasha kuchangia vifaa tiba wodi ya wazazi Mwananyamala


Na Winfrida Mtoi, Mtanzania Digital

JK Mzungu Fitness Gym imeandaa tamasha la michezo kwa lengo la kuchangia vifaa katika wodi ya wazazi ya hospitali ya Rufaa ya Mwananyamala, jijni Dar es Salaam.

Tamasha hilo linalotarajiwa kufanyika Oktoba 19, 2024 kwenye fukwe za Msasani, litashilikisha mbio za 5km – 10km na michezo mbalimbali.

Akizungumza na waandishi wa habari leo Septemba 17, 2024, Mmiliki wa Gym hiyo, Janeth Kimambo amesema kauli mbiu ya tamasha hilo ni Afya ya Mama ni Afya ya Familia kutokana na kutambua umuhimu wa afya mama na mtoto.

“Tumechagua hospitali hii kwa kuwa tunatambua thamani ya mama na mtoto kwa kuwasaidia kununua vifaa ambavyo vitawasaidia wanawake wajawazito pamoja na watoto, amesema Janet.

Amesema pamoja na michezo itayokuwepo katika tamasha hilo, washiriki watapata fursa ya kupima presha sukari pamoja na kupewa ushauri kutoka kwa madaktari bingwa wa hospitali hiyo.

Ametoa wito kwa taasisi nyingine kuwaunga mkono ili waweze kufanikisha tukio hilo na kusisitiza watu wafanye mazoezi kwa bidii kwa ajili kulinda afya zao.

Naye Daktari Bingwa wa Magonjwa ya Wanawake na afya ya uzazi, Luzango Maembe amesema anaishukuru Gym hiyo kwa kuamua kuwasaidia kununua vifaa hivyo ambavyo vitapunguza vifo vya mama mjamzito pamoja na watoto.

“Kwa niaba ya Hospitali ya Mwananyamala tunamsukuru mmiliki wa Gym hii kwa kufanya jambo hili kwani mazoezi ni sehemu ya tiba kwani kwa sasa kuna magongwa mengi yasiyoambukiza ambayo yanasababishwa na maisha ya watu, hili limekuja wakati muafaka wa kupunguza vifo vya mama na watoto, amesema Maembe.

Amese kama madaktari watakuwa na muda wa kutoa tiba na ushauri kwa washiriki wote ili waweze kupata afya kwa ajili ya kuimarisha miili yao na kuahidi kuwaunga mkono katika tamasha hilo.

Kwa upande wake mwakilishi i wa Shirikisho la Riadha Tanzania (RT), Filex Chunga amesema siku hiyo watakimbia mbio kuanzia kilometa 5-10.

“Kwa upande wetu tutahakikisha tunasimamia jambo hilo kwani kupitia michezo tumeweza kufanya tamasha hilo,amesema Chunga.

- Advertisement -

Related Articles

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Stay Connected

90,904FansLike
214,997FollowersFollow
589,000SubscribersSubscribe

Latest Articles