Na MWANDISHI WETU – Dar es Salaam    |   Â
RAIS mstaafu Jakaya Kikwete amekwenda nchini Zimbabwe kumwakilisha Rais Dk. John Magufuli katika sherehe za kumwapisha Rais mteule wa nchi hiyo, Emmerson Mnangagwa.
Taarifa ya Magufuli kuwakiliswa na Kikwete, ilitolewa kwa vyombo vya habari jana na Mkurugenzi wa Mawasiliano ya Rais-Ikulu, Gerson Msigwa, akiwa Chato mkoani Geita.
Ilieleza kuwa katika safari hiyo, Kikwete, atafuatana na Makamu Mwenyekiti wa Chama Cha Mapinduzi (CCM) Bara, Philip Mangula na Mwenyekiti wa Chama cha UDP, John Cheyo.
[embedyt] https://www.youtube.com/watch?v=7-TOv62_fWo[/embedyt]
Sherehe za kuapishwa Mnangagwa zinatarajiwa kufanyika mjini Harare leo katika Uwanja wa Michezo wa Taifa.
Mnangagwa anaapishwa kuongoza Zimbabwe baada ya kushinda katika Uchaguzi Mkuu uliofanyika Julai 30, mwaka huu akipokea kijiti kutoka kwa aliyekuwa Rais wa nchi hiyo, Robert Mugabe.