31 C
Dar es Salaam
Thursday, December 19, 2024

Contact us: [email protected]

JINSI MPANGO MKAKATI UNAVYOSAIDIA KAMPUNI KUJIENDESHA KIBIASHARA

Mkutano wa Benki ya Dunia.
Mkutano wa Benki ya Dunia.

Na BAHEBE JOSEPH,

NI ukweli usiopingika kwamba kampuni au taasisi zote huendeshwa kwa mpango mkakati na nafasi ya kampuni yoyote katika kujiendesha kibiashara huanzia katika Idara ya Rasilimali Watu, kwamba ndiyo idara pekee inayosimamia rasilimali muhimu sana kuliko zote duniani kwa kusimamia kuanzia kuajiri, kusimamia kazi, nidhamu, uzalishaji, maendeleo ya mfanyakazi na kazi, kuleta motisha, kumjengea uwezo mfanyakazi kwa maana ya mafunzo na mengine mengi.

Katika hali ya kampuni kujijengea uwezo wa kushindana na washindani wake kibiashara, njia na nafasi nzuri ya kushinda huanzia katika mpango mkakati kwa maana ya kuzingatia dira, mbinu na malengo mahususi ya uanzishwaji wa kampuni au taasisi ili iweze kufanya vizuri, vitu hivi vitatu ndivyo ambavyo huanza kwa kutoa mwongozo katika kikao cha mpango kazi, ambayo tunaamini kampuni au taasisi yoyote ile huwa na malengo ya muda mrefu na mfupi.

Sasa katika kutaka kufikia malengo, kampuni hutakiwa kugawa malengo yake katika mwaka mmoja mmoja ili kuweza kutoa nafasi ya idara zote ndani ya kampuni, taasisi kuja na mipango mikakati yao ambayo kimsingi Mkurugenzi au Ofisa Mtendaji Mkuu hutoa malengo kwa kuwaeleza wakuu wa idara zote kwa maana ya menejimenti kwa kuwaeleza yanayotakiwa kufikiwa kwa mwaka husika.

Baada ya kufanya hivyo, idara hutumia nafasi hiyo kwa kukaa na kupanga mikakati ya jinsi ya kufanikisha malengo hayo kwamba kila mkuu wa idara hufanya kikao cha idara yake na kuruhusu mawazo mbalimbali yanayoweza kuwasaidia kufikia malengo hayo pamoja na kuzingatia changamoto mbalimbali ambazo zitatakiwa kutafutiwa majibu.

Lengo kuu ni kuhakikisha kila mfanyakazi anatumia nafasi yake kufanikisha malengo makuu ya kampuni, baada ya idara kukamilisha mpango mkakati wao ambao huambatana na bajeti itakayoweza kusaidia kufikiwa kwa malengo hayo.

Idara zote zikishamaliza kuandaa mpango mkakati wao na kuwasilisha katika kikao kikuu cha mpango mkakati utakaohusiha idara zote, idara ya rasilimali watu ikiwa msimamizi wa zoezi lote la vikao hivyo kwa kuhakikisha idara zote zimeandaa mpango mkakati wao. Kisha huitishwa kwa kikao kikubwa cha kampuni, taasisi na kujadili mbinu na mikakati mbalimbali ambayo kila idara imeandaa.

Katika kikao hiki huongozwa na kitu kinaitwa SWOT Analysis ambayo tafsiri yake ni kampuni kujiangalia katika maeneo haya ya uwezo, udhaifu, fursa na tishio la kibiashara.

Wakuu wote wa idara huanza kuelezea mwanzo mpaka mwisho jinsi walivyojipanga kufikia malengo yaliyokusudiwa kwa kuwaeleza menejimenti mbinu na mikakati na kutoa nafasi kwa michango ambayo itawasaidia kuboresha maeneo yatakayoonekana yana udhaifu na michango yote hupokelewa na kufanyiwa marekebisho kama timu moja iliyokusudia kufanikisha malengo makuu ya kampuni, baada ya wakuu wa idara zote kukamilisha zoezi hilo la uwasilishaji.

Kikao hupitisha na hujumuisha mipango yote kwa kuiweka pamoja na kutumika kama kiongoza njia (roadmap) ya mafanikio ya kampuni au taasisi.

Idara ya rasilimali watu ndiyo huwa ya mwisho kwa kuhitimisha baada ya kuona na kujua mahitaji ya idara nyingine lengo ni kuhakikisha inatengeneza mpango kazi utakaowezesha kuunga mkono maeneo yote yaliyotolewa na kuelezewa na idara nyingine. Ikumbukwe kazi kubwa ya idara hii ni kuwawezesha wafanyakazi kutimiza malengo yaliyokusudiwa kwa kuwajengea mazingira mazuri na kutimiza mahitaji yao muhimu ili kuweza kutoa nafasi sawa ya kuwapima wafanyakazi kwa haki na usawa ili kila mmoja aweze kuona.

Katika hali ya utekelezaji wa mpango kazi idara ya rasilimali watu huandaa mpango wa upimaji wa utendaji kazi kwa maana ya (Perfomance Management Reviews system) kwa kuhusisha idara zote kwamba mkuu wa idara kwa kushirikiana na idara ya rasilimali watu hupanga malengo kwa kila mfanyakazi mmoja mmoja ndani ya idara yake kwa kumwita na kumpa fursa ya kujipima kwa kuweka malengo anayoona anaweza kuyafikia angalau ndani ya miezi sita.

Mkuu wake wa kazi hutoa mapendekezo pale anapoona malengo ya mfanyakazi hayajakaa vizuri na kuongeza pale inapowezekana.

Na katika kuweka malengo haya kwa maana ya mkuu wa idara lazima ahakikishe malengo hayo yanapimika na kuhesabika  katika kile kinachojulikana kama ‘Smart objectives’ yaani idara ya rasilimali watu husimamia mpango huo kwa idara zote na kuhakikisha kila mfanyakazi anahusishwa ipasavyo.

(Itaendelea wiki ijayo.) j[email protected]

- Advertisement -

Related Articles

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Stay Connected

90,904FansLike
214,997FollowersFollow
592,000SubscribersSubscribe

Latest Articles