24.2 C
Dar es Salaam
Friday, November 15, 2024

Contact us: [email protected]

JET kupiga vita umasikini, kuutokomeza ujangili

 MWANDISHI WETU

UMASIKINI unatajwa kama miongoni mwa sababu zinazo kwamisha mapambano dhidi ya ujangili. Wadau wa masuala ya wanyamapori wanabainisha kwa kadiri umasikini unavyo shamiri, ndivyo jamii inavyoingiwa na tamaa ya kushirikiana na majangili.

Imebainika majangili hutumia mbinu mbalimbali, ikiwa ni pamoja na kuwalipa fedha watu wanaoweza kuwasaidia kufanikisha malengo yao.Katika kuhakikisha mapambano dhidi ya ujangili yanafanikiwa kwa asilimia kubwa, njia pekee ni kutokomeza umasikini hasa kwa jamii inayozunguka hifadhi.

Miongoni mwa wadau walioyasema hayo, ni Mwenyekiti wa Chama cha 

Waandishi wa Habari za Mazingira Tanzania (JET), Dk. Ellen Otaru alipozungumza wakati wa mafunzo kwa waandishi wa habari kutoka vyombo mbalimbali nchini, yaliyofanyika hivi karibuni kwa njia ya mtandao. 

Dk. Otaru alisisitiza vita hiyo, inapaswa kushirikisha wadau mbalimbali muhimu, wakiwamo waandishi wa habari, watunga sera na Wizara ya Maliasili na Utalii. Alisema waandishi wa habari bado wana jukumu kubwa katika suala hilo,hasa kusambaza elimu kupitia majukwaa mbalimbali yanayotumika kutoa na kupokea taarifa. Alisema katika mapambano hayo, ni vema watoto nao wakashirikishwa kikamilifu katika hatua muhimu za vita dhidi ya ujangili haswa kupitia programu maalumu shuleni, zikiwamo za ujasiriamali. Exper Pius ambaye ni mtaalamu wa usimamizi wa Maliasili na Sera kutoka mradi wa USAID Protect, alisema kupiga vita ujangili, baadhi ya sekta kama vile mashirika ya ndege na bandari zina nafasi kubwa kwani wa ndio milango mikubwa inayotumika kupitisha viungo vya wanyamapori. 

Mtaalamu wa Mazingira wa Chuo Kikuu cha Dar ss Salaam, Dk. Elikana Kalumanga,alisema ili kuhifadhi mifumo ya ikolojia, ni vema watunga sera wawe wanaongea na kukubaliana juu ya mambo ya msingi katika masuala haya. 

Pia Kuwe na majadiliano ya kitaalamu baina ya wanasayansi ambayo yataleta tija pamoja na waandishi wa habari kuwa sehemu ya majadilano kuanzia mwanzo hadi mwisho ili waweze kuendelea kuifahamisha jamii masuala haya kwa ufasaha zaidi. 

Akifafanua juu ya uhusiano ulipo kati ya vita dhidi ya ujangili na suala zima la Utalii, Moses Njole, Mwalimu wa utalii wa Chuo cha Mweka, mkoani Kilimanjaro, alisema utalii ni moja ya sekta zinazokuwa kwa haraka sana nchini na duniani kote, ambapo inachangia pato la taifa la Tanzania kupitia fedha za kigeni kwa asilimia 25, pia inatoa fursaya ajira milioni mbili. 

John Chikomo, Mkurugenzi wa JET amesisitiza kuwa bado wameendelea na watatoa zaidi mafunzo kwa waandishi lengo likiwa ni kuhakikisha chama hicho kinaendelea kuwajengea uwezo na kuwa na uelewa mpana wa kuandika habari za uhifadhi na mazingira kwa ujumla. 

JET wamekuwa wakiandaa mafunzo mbalimbali ya masuala ya uhifadhi wa wanyamapori kwa waandishi wa habari za mazingira, kwa kipindi hiki ambapo bado watu wanachukua tadhari kubwa dhidi ya ugonjwa wa COVID-19 waliendesha mafunzo ya siku mbili kwa njia ya mtandao, mafunzo hayo yaliwakutanisha waandishi kutoka vyombo mbalimbali vya habari pia kutoka mikoa tofauti chini ya ufadhili wa Shirika la Internews.

- Advertisement -

Related Articles

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Stay Connected

90,904FansLike
214,997FollowersFollow
591,000SubscribersSubscribe

Latest Articles