RAYMOND MINJA IRINGA
Jeshi la magereza mkoani Iringa linatarajia kujenga uwanja mkubwa na wa kisasa ili kutatua changamoto ya upungufu wa viwanja vya mazoezi na michezo mbalimbali ikiwamo ligi ya soka Tanzania bara.
Ujenzi wa uwanja huo utajumuisha uwanja wa mpira wa kikapu, volibo na uwanja wakuruka kamba ambapo kwa awamu ya kwanza utagarimu Sh. miloni 44.
Akizungumza na Mtanzania Mkuu wa Magereza Mkoa wa Iringa, ASP Eduthi Mbogo amesema matayarisho ya ujenzi wa uwanja huo yameshaanza kwa kutumia nguvu kazi waliyonayo kutoka gerezani.
Mbogo amesema uwanja huo ni moja ya kitega uchumi kwani matamasha mbalimbali yatafanyika hapo na msimu wa ligi kuu utakapoanza timu mbalimbali zitakwenda kuweka kambi na wao kuingiza kipato kitakachowasaidia kuendesha shunguli mbali mbali za magereza.
“Ujenzi wa uwanja huu wa kisasa pamoja na ujenzi wa sehemu ya kupumzikia watu haya ni maelekeo kutoka kwa Kamishina Mkuu wa Magereza Tanzania, Suleman Mzee kuwa jeshi la magereza linatakiwa kujitegemea kwa kila kitu hivyo tumeamua kujenga miradi mbalimbali huu ukiwa mmoja wapo ili tupate fedha tutakazotumia kununulia wafungwa wetu chakula na vitu vingine,” amesema Mbogo.