27.2 C
Dar es Salaam
Tuesday, April 16, 2024

Contact us: [email protected]

JELA MIAKA 20 KWA KUKUTWA NA KILO 110 YA NYAMA YA KIBOKO

Mahakama ya Wilaya ya Mpanda mkoani Katavi imemhukumu Mkazi wa Kijiji cha Itenka, Wilaya ya  Mpanda kifungo cha miaka 20 jela baada ya kutiwa hatiani kwa kukutwa na nyama ya kiboko zaidi ya kilo 110 yenye thamani y ash milioni 2.3.

Hakimu Mkazi Mfawidhi wa mahakama hiyo, Chiganga  Ntengwa ametoa hukumu hiyo leo Ijumaa Desemba 8, baada ya mahakama kuridhika na ushahidi uliotolewa  mahakamani hapo na upande wa mashtaka uliokuwa ukiongozwa na Mwanasheria wa Serikali, Flavian Shio.

Akisoma hukumu hiyo Hakimu Chiganga  amesema kutokana na ushahidi uliotolewa mahakamani  hapo na upande wa mashtaka ambao ulikuwa na  mashahidi watano na mshitakiwa hakuwa na shahidi yeyote.

“Mahakama pasipo shaka yoyote imemuona mshtakiwa   ana hatia kupitia Kifungu cha Sheria Namba 86 (1) na (2) cha Sheria ya Wanyamapori Namba 5 ya  mwaka  2009,” amesema Hakimu Chiganga.

Awali ilidaiwa mahakamani hapo kuwa mshitakiwa  Omary Maganga alitenda kosa hilo Oktoba 10 mwaka jana ambapo alikamatwa akiwa ndani ya Hifadhi ya Taifa ya  Katavi  akiwa na nyama ya  kiboko  yenye  uzito wa kilo 118 yenye  thamani ya  Sh milioni tatu.

- Advertisement -

Related Articles

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Stay Connected

90,904FansLike
214,997FollowersFollow
586,000SubscribersSubscribe

Latest Articles