MWANAMITINDO maarufu nchini Marekani, Janice Dickinson, amedai ameshindwa kuacha kuvuta sigara.
Mrembo huyo ambaye anasumbuliwa na saratani ya matiti, alifanyiwa upasuaji hivi karibuni na madaktari na
kutakiwa aachane na sigara, lakini anaonekana kushindwa baada ya juzi kukutwa akivuta tena.
Hata hivyo, kupitia akaunti ya Instagram, mrembo huyo amedai kwamba anashindwa kuacha kuvuta sigara.
“Sio kama sipendi kuacha kuvuta sigara, lakini ni kwamba nashindwa, nikikaa muda mrefu bila kuvuta najisikia
vibaya na ndio maana naona bora niendelee.”