25 C
Dar es Salaam
Saturday, November 16, 2024

Contact us: [email protected]

Janeth Masaburi ahamasisha nishati mbadala kulinda mazingira

Na Mwandishi Wetu, Mtanzania Digital

Mbunge wa Viti Maalumu Mkoa wa Dar es Salaam, Janeth Masaburi amewataka mama na baba lishe kutumia nishati mbadala na kuachana na matumizi ya kuni na mkaa ili kulinda mazingira.

Masaburi ambaye ni mbunge kupitia kundi la wanawake ametoa ushauri huo Desemba 5,2023 alipofanya ziara ya kukagua miradi ya maendeleo katika Kata za Vingunguti na Kisukuru zilizoko jimbo la Segerea ambako pia aligawa majiko ya gesi kwa mama lishe.

Amesema matumizi ya kuni na mkaa yamesababisha uharibu wa mazingira na mabadiliko ya tabia nchi kutokana na ukataji miti katika maeneo mbalimbali ya nchi.

“Mheshimiwa Rais Samia anafanya jitihada kubwa kuhakikisha mazingira ya nchi yetu yanaendelea kulindwa, na sisi kama wasaidizi wake tunapita kuwaelimisha umuhimu wa kutumia nishati mbadala ili tuendelee kuwa na mazingira bora. Miti ikikosekana hatutakuwa na mvua na athari zitakuwa kubwa zaidi,” amesema Masaburi.

Mmoja wa mamalishe katika eneo la Kisukuru, Naomi Japhet, amemshukuru mbunge huyo kwa kumpatia elimu ya matumizi ya nishati mbadala na jiko la gesi na kuahidi kuacha kutumia kuni.

Mbunge huyo pia alitembelea machinjio ya Vingunguti na kusema Rais Samia amefanya kazi kubwa ya ujenzi wa miradi mbalimbali ya maendeleo ikiwemo machinjio hayo na kuwataka wananchi kuendelea kumuunga mkono.

Naye Diwani wa Kata ya Vingunguti ambaye pia ni Meya wa Halmashauri ya Jiji la Dar es Salaam, Omary Kumbilamoto, amesema ujenzi wa eneo la kuuzia utumbo uliogharimu Sh milioni 520 umewezesha kitoweo hicho kuuzwa katika mazingira bora yanayozingatia afya za wa

- Advertisement -

Related Articles

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Stay Connected

90,904FansLike
214,997FollowersFollow
591,000SubscribersSubscribe

Latest Articles