27.1 C
Dar es Salaam
Thursday, January 2, 2025

Contact us: info@mtanzania.co.tz

Janet Jackson apumzika muziki

Janet JacksonNEW YORK, MAREKANI

DADA wa marehemu Michael Jackson, Janet Jackson, ameamua kupumzika kufanya mizunguko ya maonyesho yake ya kimuziki kwa ajili ya familia yake.

Mrembo huyo aliweka video yake katika akaunti ya Instagram, akieleza lengo la kupumzika kimuziki.

“Sina mpango wa kufanya shoo hivi karibuni kutokana na mipango na mume wangu ya kuitumikia familia yangu, nimekuwa nikizunguka kufanya muziki sehemu mbalimbali na kukaa mbali na familia yangu, lakini kwa sasa nataka kutulia,” alisema Janet kupitia video hiyo.

Hata hivyo, daktari wa msanii hiyo alimtaka apumzike kwa kipindi kirefu kwa ajili ya kuimarisha afya yake.

Kutokana na tangazo hilo, baadhi ya mashabiki wake wanadai kwamba, msanii huyo ni mjamzito ndiyo maana anajipumzisha kwa muda.

- Advertisement -

Related Articles

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Stay Connected

90,904FansLike
214,997FollowersFollow
593,000SubscribersSubscribe

Latest Articles