26.7 C
Dar es Salaam
Saturday, February 24, 2024

Contact us: [email protected]

JAMHURI YAPINGA DHAMANA YA MANJI

PATRICIA KIMELEMETA NA MANENO SELANYIKA

 

UPANDE wa Jamhuri umewasilisha kiapo cha pingamizi kuhusu maombi ya dhamana katika kesi inayomkabili mfanyabiashara maarufu, Yusuph Manji (41) na wenzake watatu.

 

Uamuzi huo umekuja baada ya Mahakama Kuu Tanzania, Kanda ya Dar es Salaam, kutoa muda wa kuwasilisha pingamizi la awali dhidi ya maombi ya dhamana ya kesi ya uhujumu uchumi inayomkabili mfanyabiashara huyo na wenzake watatu.

 

Katika kesi hiyo, Mawakili wa Jamhuri, Paul Kadushi na Simon Wankyo, waliwasilisha maombi hayo jana mbele ya Naibu Msajili wa mahakama hiyo, Augustino Siani na kuiomba

kutupilia mbali maombi hayo, kwa madai kuwa mahakama haina uwezo wa kusikiliza vifungu vyenye dosari.

 

Hata hivyo, kesi hiyo imeahirishwa hadi Agosti 7, mwaka huu, kwa sababu Jaji anayesikiliza kesi hiyo, Isaya Arufani, hakuwapo.

 

Awali, Manji na wenzake, Deogratias Kisinda (28), mkazi wa Mbezi, Ofisa Rasilimali Watu (HR), Abdallah Sangey (46) mkazi wa Jangwani, ambaye ni msimamizi wa stoo na Thobias Fwele (43), mkazi wa Chanika, walipandishwa kizimbani kwa madai ya kukutwa na vitambaa vya sare za Jeshi la Wananchi Tanzania (JWTZ) isivyo halali, vyote vikiwa na thamani ya Sh milioni 236.5.

 

Washtakiwa hao wanadaiwa kujipatia bidhaa isivyo halali mnamo Juni 30, mwaka huu, katika maeneo ya Chang’ombe A Temeke, Jijini Dar es Salaam, walikutwa na askari polisi wakiwa na mabunda 35 ya vitambaa vinavyotumika kutengeneza sare za Jeshi la Wananchi wa Tanzania (JWTZ) zenye thamani ya Sh milioni 192.5, ambazo zilipatikana isivyo halali.

 

Washtakiwa hao wanadaiwa kukutwa na maofisa wa polisi katika eneo la Chang’ombe A Temeke, jijini Dar es Salaam, wakiwa na bidhaa za mabunda nane ya vitambaa vya kutengeneza sare za JWTZ zenye thamani ya Sh milioni 44.

 

Pia wanadaiwa kukutwa na mhuri wa Serikali wa JWTZ isivyo halali mnamo Juni 30, mwaka huu, ambao umeandikwa “Mkuu wa Kikosi 121 kikosi cha JWTZ” bila kuwa na uhalali na kwamba kitendo hicho kinahatarisha uchumi na usalama wa nchi.

 

Wanadaiwa kukutwa na mhuri wa Serikali wa JWTZ isivyo halali ambao umeandikwa “Kamanda Kikosi 834 KJ Makutupola Dodoma” bila kuwa na uhalali na kwamba kitendo hicho kingeweza kuhatarisha usalama wa nchi.

 

Wanadaiwa kukutwa na mhuri wa serikali ulioandikwa “Commanding Officer 835 KJ Mgambo, P.O. Box 224, Korogwe” kinyume cha sheria.

 

Wanadaiwa kukutwa na mali inayodhaniwa kupatikana isivyo halali ambayo ni namba ya gari zinazosomeka SU 383, mnamo Julai Mosi, mwaka huu.

 

Wanadaiwa kukutwa na namba ya gari inayosomeka SM 8573, kinyume cha sheria.

- Advertisement -

Related Articles

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Stay Connected

90,904FansLike
214,997FollowersFollow
583,000SubscribersSubscribe

Latest Articles