29.9 C
Dar es Salaam
Sunday, November 17, 2024

Contact us: [email protected]

Jaji Mgeta aeleza kigogo wa Serikali ‘alivyomtikisa’

Na Esther Mnyika, Mtanzania Digital

Jaji aliyemaliza muda wake wa kuitumikia Mahakama, Jaji John Mgeta amesema katika kazi yake ya utumishi kama Jaji hatasahau namna ambavyo kigogo wa Serikali alichana hukumu mbele yake.

Jaji Mgeta ameyasema hayo leo Mei 4, 2023 muda mfupi baada ya hafla ya kuagwa yeye na majaji wengine wawili iliyofanyika Mahakama Kuu Kanda Masjala ya Dar es Salaam.

Jaji Mgeta amelitaja tukio hilo kama moja hya changamoto kubwa aliyowahi kukutana nayo katika utendaji wake.

Miongoni mwa changamoto nilizokutana nazo ni kusimamia kesi ya aliyekuwa kigogo wa Serikali na kushindwa kesi kwa kigogo huyo. Katika shauri hilo kigogo wa serikali alishindwa kesi lakini nilipopeleka maamuzi ya mahakama aliyadharau na kuamua kuchana karatasi ya hukumu, kitendo hiki kiliniumiza sana na nilikosa furaha, lakini nashukuru baadae serikali ilisimama na kutekeleza kile kilichoagizwa na mahakama,”amesema Jaji Mgeta.

Awali, akizungumza katika hafla ya kuwaaga majaji hao, Jaji Kiongozi Mustapha Siyani amesema wananchi hawapaswi kuwa na wasiwasi na mahakama kwani ni huru na inatoa haki.

Jaji Siyani amewataja majaji hao waliomaliza muda wao wa utumishi kuwa ni Jaji Sekela Moshi, Jaji Beatrice Mtungi na Jaji John Mgeta ambapo amesema kuwa kipindi chote cha kazi kwa majaji hao walikuwa wanafanya kazi kwa weledi.

Amesema mbali na kuchapa kazi pia waliomaliza muda wao na wenye utii kwa kila mtu na kwamba kuondoka kwao ni pengo.

“Wananchi wakikosa imani na mahakama kila mtu atachukua sheria mkononi, na nchi yoyote duniani lazima iwe na mahakama, hivyo tuna mahakama nchi nzima zipo kwa ajili ya kuwasikiliza wananchi,” amesema Jaji Siyani.

Amesema kitendo cha kumaliza muda wao wa kazi kisheria ni alama tosha ya kuweza kuigwa kwa watumishi ili kuleta ufanisi katika kazi yao.

“Tunawakumbuka kwa bidii yenu ya kazi lakini na namna bora ya uongozi kwa kutatua kesi mbalimbali bila kujali ukubwa wake,” ameongeza Jaji Siyani.

Aidha, amesoma wasifu wa viongozi hao ambapo amesema wote walikuwa wamejaaliwa ujuzi katika kuandika hukumu pamoja hekima wanapokuwa na watu.

- Advertisement -

Related Articles

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Stay Connected

90,904FansLike
214,997FollowersFollow
591,000SubscribersSubscribe

Latest Articles