22.8 C
Dar es Salaam
Wednesday, May 22, 2024

Contact us: [email protected]

Fainali Bonnah Segerea Cup kupigwa Jumapili

Na Mwandishi Wetu, Mtanzania Digital

Fainali za mashindano yaliyoandaliwa na Mbunge wa Jimbo la Segerea, Bonnah Kamoli zitafanyika Jumapili wiki hii katika uwanja wa Shule ya Msingi Tabata.

Mashindano hayo yaliyoanza kutimua vumbi Desemba 3 mwaka jana yanashirikisha timu 64 za soka zikiwemo 61 za mitaa yote inayounda jimbo hilo, timu ya umoja wa bodaboda, timu ya umoja wa bajaji na timu ya UVCCM – Jimbo la Segerea.

Pia kuna timu 13 za mchezo wa rede ambapo kila kata imetoa timu moja.

Akizungumza na Waandishi wa habari, Katibu wa mbunge huyo, Lutta Rucharaba, amesema katika fainali hizo timu ya Bonyokwa itavaana na Kisiwani wakati katika mchezo wa rede Buguruni watavaana na Mnyamani.

“Mheshimiwa mbunge ameandaa mashindano haya kwa lengo la kuibua vipaji vya vijana kwa sababu kupitia michezo wanaweza kupata fursa mbalimbali kama za ajira na pia kuimarisha afya zao,” amesema Rucharaba.

Amesema mgeni rasmi katika fainali hizo anatarajiwa kuwa Mwenyekiti wa UVCCM Taifa, Mohamed Ally Kawaida.

Kuhusu zawadi amesema mshindi wa kwanza atapata Sh milioni 5
wakati mshindi wa pili atapata Sh milioni 3 na mshindi wa tatu Sh milion 2.

Kwa mujibu wa Lutta, katika fainali hizo pia vilabu zaidi ya 200 vya Jogging kutoka Dar es Salaam na Pwani vitashiriki na kwamba kutakuwa burudani kutoka kwa wasanii mbalimbali wa muziki wa kizazi kipya.

- Advertisement -

Related Articles

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Stay Connected

90,904FansLike
214,997FollowersFollow
587,000SubscribersSubscribe

Latest Articles