26.1 C
Dar es Salaam
Friday, January 3, 2025

Contact us: info@mtanzania.co.tz

Jaja asaini miaka miwili Yanga

Santos Santana ‘Jaja’
Mchezaji wa Yanga Geilson Santos Santana ‘Jaja’ akipokea nakala ya mkataba wake kutoka kwa Katibu Mkuu wa yanga, Beno Njovu, jana baada ya kusaini kuichezea timu hiyo kwa miaka miwili.

NA MWALI IBRAHIM, DAR ES SALAAM

KLABU ya Yanga jana imeingia mkataba wa miaka miwili na mshambuliaji Mbrazil, Geilson Santos Santana ‘Jaja’,  kuichezea timu hiyo, ambapo mkataba huo utafikia kikomo mwaka 2016.

Jaja alijiunga na kikosi hicho wiki iliyopita ambapo alianza kupewa mazoezi ya peke yake kwa ajili ya kumfanya azoee hali ya hewa, huku wakiwa katika uangalizi wa kiwango chake kabla ya kupewa mkataba huo.

Akizungumza Dar es Salaam jana, Katibu Mkuu wa Yanga, Beno Njovu, alisema usajili huo wa Jaja unaifanya timu hiyo kuwa na wachezaji wawili wa kimataifa waliowasajili msimu huu, wote wakitokea nchini Brazil, akiwemo Andrey Coutinho.

“Kazi yetu uongozi ni kutekeleza maelekezo ya kocha mkuu pamoja na benchi la ufundi, walitoa mapendekezo ya usajili kabla hawajaanza kazi na mengine baada kuwasili, yote tunajitahidi kuyatekeleza ili kila kitu kiende safi,” alisema.

Alisema mchezaji huyo ataanza kuitumikia timu kwenye michuano ya Klabu Bingwa Afrika (CECAFA), inayotarajia kuanza Agosti 8 nchini Rwanda, kabla hawajaanza Ligi Kuu Septemba 20.

Alisema, Jaja alizaliwa  Septemba 21 mwaka 1985 na kukulia katika mji wa Aracaju, nchini Brazil, mpaka anasajiliwa na timu ya Young Africans alikuwa akiichezea timu ya Itabaina FC iliyopo nchini Brazil.

- Advertisement -

Related Articles

1 COMMENT

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Stay Connected

90,904FansLike
214,997FollowersFollow
593,000SubscribersSubscribe

Latest Articles