28.2 C
Dar es Salaam
Friday, November 15, 2024

Contact us: [email protected]

JAFO APOKEA MPANGO WA KUENDELEZA USAFIRI DAR

NA Aziza Masoud, Dar es Salaam        |       


WAZIRI wa Nchi, Ofisi ya Rais, Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa (Tamisemi), Seleman Jafo, amepokea Mpango wa Kuendeleza Usafiri Dar es Salaam (MRT) wenye thamani ya Sh bilioni 21.4.

Mpango huo unatoa muongozo wa utekelezaji wa mradi huo unaofadhiliwa na Shirika la Maendeleo la Japan (Jica) unaelekeza namna ujenzi wa miundombinu mbalimbali ya usafiri ukiwamo wa reli, barabara na mabasi na utekelezaji wake utafanyika kwa awamu tatu kati ya mwaka  2018 na mwaka 2040.

Akizungumza Dar es Salaam juzi wakati wa kupokea mpango huo, Jafo, alisema  utekelezaji wake unafanyika baada ya Tanzania kutuma maombi katika Serikali ya Japan mwaka 2005 lengo likiwa ni kupunguza msongamano jijini hapa.

“Mpango huu una lengo mahsusi la kuboresha Jiji la Dar es Salaam na kuondoa msongamano katika huduma ya usafiri kwa wananchi,” alisema Jafo.

Alisema ramani za utekelezaji wa mpango huo zinaonyesha uwepo wa barabara kubwa kwa kila eneo lenye makazi ya watu na kutakuwa na utaratibu wa watu kutumia usafiri wa jumla kuingia katikati ya jiji.

Pia alisema ramani inaonyesha kutakuwa na reli kutoka Daraja la Surrender hadi Tegeta itakayowasaidia wananchi wa maeneo hayo kufika haraka katikati ya mji.

“Nilikuwa naomba mnapoanza utekelezaji kama itawezekana kipaumbele kiwe hii reli ikiwezekana isiishie Tegeta tu ifike hadi Bunju, maeneo haya yaa watu wengi ambao wanaingia katika ya jiji,” alisema Jafo.

Alisema ifikapo mwaka 2040 Dar es Salaam itakuwa na watu 12,000,000 na idadi hiyo haitakidhi miundombinu ya sasa.

“Foleni zinazosababishwa na ukosefu wa miundombinu zinakwamisha shughuli za kiuchumi, wataalamu wanasema tunapoteza fedha nyingi kwa sababu watu hawafiki maeneo ya uzalishaji kwa muda lengo letu sasa ni kuondoa hii,” alisema.

Jafo alisema utekelezaji wa mradi huo na mengine ni malengo ya Serikali kuiboresha Dar es Salaam baada ya kuhamia Dodoma.

Kwa upande wake, Mwakilishi Mkuu wa Jica hapa nchini, Toshio Nagase, alisema   utekelezaji wa mradi huo unakusudia kuwasaidia wananchi wa Dar es Salaam  katika suala la usafiri ambalo ni tatizo.

- Advertisement -

Related Articles

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Stay Connected

90,904FansLike
214,997FollowersFollow
591,000SubscribersSubscribe

Latest Articles