Izzo Bizness: Sitoi wimbo bila mama kuukubali

0
1047

IzzomNA CHRISTOPHER MSEKENA

MKALI anayefanya vizuri kwenye muziki wa kizazi kipya nchini, Emmanuel Simwinga ‘Izzo Bizness’, amesema kabla hajatoa wimbo ni lazima ampe mama yake ausikilize ndiyo aupeleke redioni.

Izzo alisema tabia hiyo aliianza baada ya kutoa wimbo wake wa kwanza wa ‘Biziness’ na alipoupitisha huwa na mafanikio makubwa, ndiyo maana anaendelea na hali hiyo hadi sasa.

“Huwa namtumia nyimbo mbili kisha yeye anachagua upi niutoe, nipo tofauti na wasanii wengi ambao kabla hawajatoa wimbo huwa wanawapa watangazaji, madj na wadau wengine wa muziki, lakini mimi mama yangu ndiyo amekuwa mchaguzi wangu wa nyimbo zangu,” alisema Izzo Bizness.

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here