26.9 C
Dar es Salaam
Friday, January 3, 2025

Contact us: info@mtanzania.co.tz

ISRAEL YAADHIMISHA MIAKA 70 YA KUUNDWA KWAKE

TEL AVIV, ISRAEL


WAZIRI Mkuu wa Israel, Benjamini Netanyahu, ametumia maadhimisho ya miaka 70 tangu kuundwa kwa taifa hilo kuwaonya maadui wao.

Akizindua rasmi sherehe za maadhimisho hayo, Netanyahu, aligusia juu ya uhusiano bora na baadhi ya mataifa ya Kiarabu, akiionya Iran kuwa yu tayari kushirikiana na wale wanaotaka tu amani.

Katika sherehe hizo zilizoanza kwa tukio la kuwashwa mwenge, Netanyahu alisema Israel bado inaendelea kuandamwa na majirani zake, ambao wengi wao wanaonekana kutokubaliana na uwepo wa taifa hilo na kuonya hawatamwacha yeyote anayekwenda kinyume.

Kwa upande mwingine, Rais Donald Trump wa Marekani, kupitia ukurasa wa twitter, amemtakia Netanyahu maadhimisho mema ya kumbukumbu ya miaka 70 tangu kuundwa kwa taifa la Israel.

Trump aliongeza kuwa anatarajia kuuhamishia rasmi ubalozi wa Marekani mjini Jerusalem mwezi ujao.

- Advertisement -

Related Articles

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Stay Connected

90,904FansLike
214,997FollowersFollow
593,000SubscribersSubscribe

Latest Articles