26.9 C
Dar es Salaam
Friday, January 3, 2025

Contact us: info@mtanzania.co.tz

Isha Mashauzi aungana na Mwakinyo Mtata Mtatuzi

Na Winfrida Mtoi, Mtanzani Digital

Mwanamuziki wa miondoko ya taarabu, Isha Mashauzi atakuwa miongoni mwa watakaoshudia a pambano la ngumi la bondia Hassan Mwakinyo lililopewa jina la Mtata Mtatuzi.

Mwakinyo anatarajiwa kupanda ulingoni Januari 27, 2024 kuzichapa na Mbiya Kanku raia wa DR Congo pambano la ubingwa wa WBO Afrika litakalopigwa Amani Complex Indoor Arena, Zanzibar.

Akizungumza na waandishi wa habari wakati wa kuelekea visiwani humo, Isha amesema alikuwepo Ubungo Plaza Desemba 26, 2023 na kushudia vitasa hasa kwa wanawake hivyo kuamua kwenda tena Zanzibar kuona burudani hiyo.

Ameeleza kuwa lengo ni kupeana sapoti kwa sababu ngumi na muziki vyote vinakwenda pamoja.

“Ngumi ni muziki na muziki ni ngumi. Zamani tulikuwa tunaamini kwamba wanaopenda michezo hii ni wanaume tu na ni hatari lakini sasa hivj hata watoto wa kike wanafanya vizuri ndiyo maana nikaamua kuja kusapoti,” amesema Isha.

Amesema kwa hali ilivyo Tanzania itafika mbali kupitia mchezo wa ngumi, huku akiwataka mashabiki kununua tiketi ili kushuhudia mapambano hayo.

Kwa upande wake Mwakinyo amesema ameshakamilisha maandalizi na kutamba kuwa yeye ni bondia mkubwa hana mpinzani nchini.

- Advertisement -

Related Articles

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Stay Connected

90,904FansLike
214,997FollowersFollow
593,000SubscribersSubscribe

Latest Articles