29.9 C
Dar es Salaam
Monday, December 16, 2024

Contact us: [email protected]

IRUWASA yakabiliwa na changamoto ya mfumo wa uondoaji maji taka

Na Ramadhan Hassan,Dodoma

MAMLAKA ya Maji safi na Usafi wa Mazingira Iringa (IRUWASA) umesema unakabiliwa na changamoto ya mfumo wa uondoaji wa majitaka ambapo hadi sasa wameweza kuwafikia wananchi kwa asilimia 6.8.

Mkurugenzi Mtendaji wa Mamlaka ya majisafi na usafi wa mazingira Iringa (IRUWASA) akizungumza na waandishi wa habari jijini Dodoma

Amesema jumla ya kaya 2,469 ndio zilizounganishwa.

Hayo yameelezwa Februari 27,2023 na Mkurugenzi Mtendaji wa Mamlaka hiyo David Pallangyo wakati akizungumza na waandishi wa habari jijini Dodoma kuhusu utekelezaji na mwelekeo wa mamlaka hiyo.

Pallangyo amesema ili kuunda mfumo huo unajumuisha uwekaji wa mabwawa saba ya kutibu majitaka, uwekaji wa mabomba makuu ya kusafirishia majitaka (trunk main) na mtadao wa mabomba ya kukusanyia majitaka (lateral sewers) yanye jumla ya urefu wa kilomita 78.6.

“Kwa maeneo ambayo mfumo wa uondoshaji majitaka haujayafikia, Mamlaka hutoa huduma hiyo kwa kutumia magari matatu (3) maalum ya kunyonya majitaka (Cesspit emptier trucks). Huduma hii pia hutolewa na sekta binafsi”amesema Pallangyo.

Hata hivyo amesema licha ya uchache wa mifumo hiyo katika Manispaa ya Iringa mifumo hiyo haipatikani kabisa katika Miji ya Kilolo na Ilula.

Akizungumzia mradi wa maji safi wa Isimani-Kilolo Pallangyo amesema IRUWASA imeshapokea Sh bilioni 7.8 sawa na asilimia 84 ya gharama ya Sh bilioni 9.2 kwaajili ya kuukamilisha.

Amesema mradi huo ulianza tarehe Aprili 15, 2020 kwa njia ya force account kwa makadirio ya gharama ya Sh bilioni 9.2 ili kukabiliana na changamoto ya maji iliyokuwepo katika maeneo ya Halmashauri ya Wilaya ya Iringa ambayo yako pembezoni mwa Manispaa ya Iringa.

Pallangyo amesema mradi huo unatarajiwa kukamilika mwezi Aprili, 2023 na kuongeza kasi ya uzalishaji wa maji kutoka lita 2,238,000 kwa siku hadi lita 4,656,000 kwa siku na hivyo kukidhi mahitaji kwa asilimia 100.

- Advertisement -

Related Articles

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Stay Connected

90,904FansLike
214,997FollowersFollow
592,000SubscribersSubscribe

Latest Articles