26.2 C
Dar es Salaam
Sunday, November 17, 2024

Contact us: [email protected]

IRAN YATISHIA KUJITOA MAKUBALIANO YA NYUKLIA

TEHRAN, IRAN


KIONGOZI mkuu wa hapa, Ayatollah Ali Khamenei, ameonyesha wasiwasi wake juu ya uwezo wa mataifa ya Ulaya kuokoa makubaliano ya nyuklia na Iran ya mwaka 2015.

Alisema hayo kutokana na mataifa  yenye nguvu ya Ulaya kukabiliwa na tisho kufuatia kujitoa kwa Marekani katika makubaliano hayo, na kwamba Iran huenda ikajitoa pia.

Khamenei amemtahadharisha Rais Hassan Rouhani kutotegemea mno uungwaji mkono kutoka mataifa ya Ulaya wakati akijikuta katika mbinyo mkali nyumbani kuhusu namna anavyoshughulikia changamoto za kiuchumi baada ya Marekani kurejesha vikwazo dhidi ya nchi hiyo, na mawaziri muhimu wakishambuliwa  bungeni.

Kufuatia kujitoa kwa Marekani katika makubaliano hayo ambayo yangedhibiti dhamira ya Iran kujipatia silaha za nyuklia, mataifa yenye nguvu ya Ulaya yamekuwa njia panda ingawa bado yanaihakikishia Iran manufaa ya kiuchumi ili kuibakisha katika makubaliano hayo.

Lakini katika matamshi yake yaliyochapishwa katika tovuti yake rasmi, Khamenei alimwambia Rouhani na baraza lake la mawaziri jana, kwamba hakuna matatizo kuendelea na  majadiliano na uhusiano na Ulaya, lakini anapaswa kuondoa matumaini kuhusu masuala ya  kiuchumi ama makubaliano ya  kinyuklia.

- Advertisement -

Related Articles

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Stay Connected

90,904FansLike
214,997FollowersFollow
591,000SubscribersSubscribe

Latest Articles