26.1 C
Dar es Salaam
Friday, January 3, 2025

Contact us: info@mtanzania.co.tz

IRAN YAMKANA RAIS TRUMP

TEHRAN, IRAN


SERIKALI ya Jamhuri ya Kiislamu ya Iran, imekanusha taarifa zilizosambaa kuwa imeomba mazungumzo na Rais wa Marekani, Donald Trump.

Kwa mujibu wa msemaji wa Wizara ya Mambo ya Nchi za Nje wa Iran, Bahram Qassemi, aliyenukuliwa na shirika la habari la nchi hiyo, IRNA amesema hakuna ukweli wowote katika taarifa za kwamba Iran iliomba kukutana na Trump wakati wa mkutano wa Baraza Kuu la Umoja wa Mataifa ambao umeanza wiki hii.

Qassemi amesema taarifa zilizomnukuu Balozi wa Marekani katika Umoja wa Mataifa, Nikki Haley, kwamba Iran inataka kukutana na Trump zimejaa uongo na zinapaswa kupuuzwa.

Aidha, Qassemi amesema Rais wa Iran, Hassan Rouhani, anatarajiwa kulihutubia Baraza Kuu la Umoja wa Mataifa wiki ijayo, lakini hakuna mpango wowote wa kuzungumza na Trump.

Mvutano umeongezeka kati ya Iran na Marekani, baada ya Trump kujiondoa katika mkataba wa kihistoria wa nyuklia kati ya Iran na mataifa yenye nguvu duniani mwezi Mei mwaka huu na kutangaza vikwazo vipya dhidi ya Iran.

>>>>>>>>>>>>>

 

Chama cha siasa kali chapata umaarufu

BONN, UJERUMANI

UCHUNGUZI mpya wa kura za maoni unaonyesha kuwa Serikali ya muungano wa Ujerumani, inapoteza uungwaji mkono wa wapiga kura, huku chama cha siasa kali za kizalendo za mrengo wa kulia cha AfD kikizidi kupata umaarufu.

Kwa mujibu wa utafiti uliofanywa na Deutschlandtrend na shirika la utangazaji la umma, ARD, umeonyesha jana kuwa chama cha AfD kimekipiku chama cha Social Democratic (SPD) ambacho ni mshirika katika Serikali ya muungano na kuwa chama cha pili chenye nguvu nyuma ya vyama ndugu vya kihafidhina vya Kansela Angela Merkel, ambavyo ni Christian Democratic Union (CDU) na Christian Social Union (CSU).

AfD kilionyesha kuimarika kwa nyongeza ya asilimia mbili tangu uchunguzi wa mwisho wa Septemba 9 na kujikusanyia asilimia 18 ikiwa ni moja zaidi ya mshirika wake mdogo wa Serikali ya muungano SPD, ambacho kilipoteza pointi moja.

Kundi la Merkel la CDU na CSU ambalo limeongoza Serikali tofauti za Ujerumani tangu 2005, pia limepoteza pointi na kufikia asilimia 28, yakiwa matokeo mabaya kabisa tokea utafiti huo ulipoanzishwa mwaka wa 1997.

- Advertisement -

Related Articles

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Stay Connected

90,904FansLike
214,997FollowersFollow
593,000SubscribersSubscribe

Latest Articles