26.1 C
Dar es Salaam
Friday, January 3, 2025

Contact us: info@mtanzania.co.tz

Infinix na Tigo wazindua HOT 4O Series yenye ufanisi wa hali ya juu

Na Mwandishi Wetu, Mtanzania Digital

Kampuni ya simu za mkononi ya Infinix, kwa kushirikiana na Tigo Tanzania zimezindua rasmi simu za Infinix HOT 40 Pro na HOT 40i zenye uwezo mkubwa ukiwamo ule wa kuendesha magemu ya simu kwa umahiri.

Aidha, simu hizo zimelenga kumfaa kila mtu kutokana na kiasi chake cha bei ambacho kinatazamiwa kuwa kati ya Sh 330,000 hadi 550,000, ikijumuisha kuongezeka kwa ufanisi makubwa katika kichakataji Processor, onyesho/Display, uwezo wa kamera na programu zake.

Wakati wa uzinduzi na vyombo vya habari uliofanyika mapema leo Desemba 16, 2023 jijini Dar es Salaam, Afisa Uhusiano wa Infinix, Aisha Karupa, alielezea kufurahishwa kwake na utendakazi wa kipekee pamoja na muonekano wa simu hiyo.

Alisema toleo hili la HOT 40 linaongoza kwa utendakazi wake wa kipekee na sifa/features muhimu, vyote vikiwa na muundo wa kuvutia huku zikiju,hisha maono ya Infinix kuongeza hali ya ubora wa juu kwa watumiaji wake, kuunganisha teknolojia ya hali ya juu na mtindo na vitendo kwa bei nzuri.

“Infinix HOT 40 Pro ina kichakataji cha Helio G99, RAM ya 8GB inayoweza kuongezeka hadi GB16 RAM, na skrini ya inchi 6.78 ambayo huleta utumiaji wa laini wakati wa kucheza michezo.

“Pia teknolojia ya kuchaji kwa haraka ya Watt 33, iliyo na ufuatiliaji wa halijoto kwa wakati sahihi. Teknolojia hii bunifu huwezesha watumiaji kuchaji betri kutoka asilimia 20 hadi asilimia 75 kwa dakika 35 tu, kuhakikisha usalama na maisha marefu ya betri kwa hadi miaka 4,” amesema Aisha na Kuongeza kuwa:

“HOT 40 Pro pia ina kamera kuu ya 108MP yenye kihisi cha HM6, kinachohakikisha kuwa picha kali na za wazi zenye pikseli 0.64-micron, hata baada ya kupunguzwa/cropping. Lenzi kuu ya 2MP hunasa picha za karibu za maumbo na maelezo tata. Kamera ya mbele iliyoboreshwa ya 32MP AI hutoa picha za kipekee za kikundi na selfies, hata katika mwanga hafifu, shukrani kwa flash yake ya juu ya mbele,” amesema Aisha.

Akizungumza wakati wa uzinduzi huo, Mtaalamu wa Bidhaa wa Tigo, Lilian Mushi alisema:”Sisi Tigo Tanzania tunayofuraha kushirikiana na Infinix katika uzinduzi wa toleo la HOT 40, ambayo ni hatua muhimu katika kufafanua upya uzoefu wa michezo kwa simu za mkononi.

“Kama washirika wa mawasiliano ya simu, tunafuraha. ili kuwapa wateja wa Tigo muunganisho usio na matatizo ili kufurahia kikamilifu uwezo wa game za simu ulioimarishwa na simu za toleo la HOT 40.

“Vipengele/features vya kisasa vya HOT 40 Pro, pamoja na mtandao wa Tigo wa kutegemewa wa 4G+ na 5G, huhakikisha kwamba watumiaji wanaweza kujiingiza katika michezo ya simu na burudani. Tunatambua HOT 40pro na HOT 40i kama uthibitisho wa kujitolea kwa Infinix katika kusukuma mipaka katika teknolojia na ubunifu, sisi kama Tigo Tanzania tunatoa bando la intaneti la GB 78 kwa wateja wa HOT 40,” amesema Lilian.

Aidha, Infinix ilipata wasaa pia wakutuhabarisha kuhusu ushirika wake na FREE FIRE, ushirikiano kati ya Infinix na Free Fire ambao unaongeza zaidi burudani ya michezo ya simu na kutoa uzoefu wa kusisimua na wa ushindani wa michezo kupitia simu kwa watazamaji.

“Infinix imeandaa mashindano kwa gamers wote mashindano hayo yanayotegemewa kuisha usiku huu wa leo mshindi kujinyakulia kitita cha shilling 1,000,000 pamoja na Infinix HOT 40 pro papo hapo,” amesema Aisha.

Infinix HOT 4O pro na HOT 4Oi zimeanza kupatikana nchi nzima tangu zilipotambulishwa huku matoleo mengine ya kampuni hiyo yakiwa bado yapo sokoni ambayo yanawawezesha wateja ujishindia zawadi za sikukuu za Christmass na Mwaka Mpya.

- Advertisement -

Related Articles

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Stay Connected

90,904FansLike
214,997FollowersFollow
593,000SubscribersSubscribe

Latest Articles