24.9 C
Dar es Salaam
Monday, November 18, 2024

Contact us: [email protected]

Ileje yajipanga kuinua ufaulu mitihani ya Kitaifa

Na Denis Sinkonde, Songwe

Wiki mbili kabla ya kuanza kwa Mwaka Mpya wa Masomo wa 2022 Wilaya ya Ileje mkoani Songwe imeanza kuweka mikakati ya kujinasua nafasi za mwisho kwenye mitihani mbalimbali ya kitaifa ya Shule za Msingi.

Hayo yamejili wakati wa kikao kilichofanyika siku mbili Desemba 28 na 29, mwaka huu kiliwahusisha Maafisa Elimu kata kutoka kata 18 zinazounda wilaya ya Ileje na walimu wakuu wa shule za msingi 85 zilizopo wilayani humo lengo likiwa ni kuwandaa kisaikolojia na kwa vitendo.

Akizungumza katika kikao hicho Mkurugenzi Mtendaji wa Halmashauri hiyo, Geofrey Nnauye, amewataka walimu kuacha kutupiana mpira badala yake wachukue hatua za kuondokana na aibu ya kushuka kitaaluma kwa miaka mitatu mfululizo.

“Wilaya ya Ileje imeshuka kitaaluma kwa miaka mitatu mfululizo, hivyo afanyeni kazi bila kusubiri kusimamiwa na mfuate miongozo ya taaluma kwani kusubiri kusimamiwa kunachangia matokeo mabaya ya elimu msingi mwaka hadi mwaka hali inayosababisha wilaya kusomeka vibaya kwa Watanzania,” amesema Nnauye.

Nnauye amewataka watalaam hao kutumia maelekezo ya kikao hicho kuhakikisha wanawatendea haki wanaileje kwa kuleta mabadiliko makubwa katika matokeo mbalimbali ya mitihani.

Upande wake, Afisa Elimu Msingi, Fikiri Mguye, amesema umoja, uwazi na ushirikiano ni silaha tosha itakayoitoa wilaya hiyo kwenye nafasi mbaya za matokeo ya mitihani mbalimbali.

“Wadau mabalimbali kutoka ngazi za juu mpaka za chini washirikishwe ili kutoa ushauri ambao utasaidia kukuza kiwango cha ufaulu na kuondoa aibu kwa wana Ileje ambao wana amini mikakati itakayowekwa itakuwa chachu ya kuifanya wilaya kuwa miongozi mwa wilaya zinazofanya vizuri kwa mkoa wa Songwe na kitaifa,” amesema Mguye.

 Akizungumza mara baada ya kikao hicho Mwenyekiti wa Maafisa hao, Phares Kibona amempongeza Mkurugenzi kwa kutambua umuhimu wa waalimu hao na kuitisha kikao cha kupanga mikakati ya kukuza kiwango cha ufaulu.

Wilaya ya Ileje iliwahi kung’ara kitaaluma miaka 20 iliyopita na sasa imeendelea kupoteza mwelekeo na kupelekea wadau mbalimbali kutokubaliana na hali hiyo.

- Advertisement -

Related Articles

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Stay Connected

90,904FansLike
214,997FollowersFollow
591,000SubscribersSubscribe

Latest Articles