28.2 C
Dar es Salaam
Friday, November 15, 2024

Contact us: [email protected]

IGP amtaka Lissu akaripoti polisi

 MWANDISHI WETU– DAR ES SALAAM

MKUU jwa Jeshi la Polisi nchini, IGP Simon Sirro, amemtaka mgombea urais wa Chadema, Tundu Lissu kwenda kuripoti kwenye Kituo cha Polisi Moshi ili aeleze alichokifanya alipokuwa mjini humo juzi.

Akizungumza jana, Sirro alisema amechukua hatua hiyo baada ya kuona matukio kadhaa yanayofanywa na viongozi wa Chadema kwamba wamekuwa na tabia ya kukaripia na kuwagombeza askari polisi.

“Nimeona mara kadhaa Tundu Lissu akigombana na viongozi wa polisi, na jana (juzi) nimeongea na kiongozi wake, Mbowe (Mwenyekiti wa Chadema, Freeman Mbowe) nimemwambia akae na watu wake wazungumze suala la utii wa sheria bila shuruti.

“Anayoyafanya Watanzania wenye hekina na wazalendo wa nchi hii wanayaona, Lissu hayuko juu ya sheria, polisi tukiamua kutimiza wajibu wetu asilalamike na chama chake,” alisema Sirro.

Alisema vyama vya siasa vyenye wagombea viko karibu 12, hivyo ajue Jeshi la Polisi limepewa wajibu wa kulinda watu na mali zao ndani ya nchi hii, yeye hana uwezo wowote wa kupambana nalo.

Sirro alisema Lissu asije akafika mahala akawa na kiburi akafikiri ana uwezo wa kupambana na polisi, kwa kuwa hicho kiburi hana.

Alisema anawaomba watu wa Chadema waache tabia hiyo na kwamba anamwelekeza Lissu aende akaripoti Kituo cha Polisi mjini Moshi ili aeleze hayo aliyoyafanya juzi.

“Lakini pia niwaombe wanasiasa na viongozi katika ngazi zote, suala la udiwani, ubunge na urais, bila amani huwezi kufanya siasa na huna uwezo wa kupambana na Jeshi la Polisi wewe kama wewe, kwa hiyo tuheshimu sheria zilizopo ili tuweze kuchagua viongozi tunaowataka.

“Lakini inaonekana kuna ajenda ya siri ambayo kuna viongozi wachache ambao wanataka fujo itokee ili uchaguzi usifanyike, hiyo nafasi hawana, uchaguzi utafanyikia na itafika mahala tutawashughulikia sana kwa mujibu wa sheria,” alisema Sirro.

- Advertisement -

Related Articles

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Stay Connected

90,904FansLike
214,997FollowersFollow
591,000SubscribersSubscribe

Latest Articles