27.2 C
Dar es Salaam
Monday, November 18, 2024

Contact us: [email protected]

ICC YAZINYOOSHEA KIDOLE ISRAEL, HAMAS

THE HAGUE, UHOLANZI


MWENDESHA mashtaka mkuu wa Mahakama ya Uhalifu wa Kivita (ICC), Fatou Bensouda, amesema huenda Israel na kundi la Hamas zimetenda uhalifu katika machafuko Ukanda wa Gaza.

Akizungumza kutokea Makao Makuu ya ICC mjini hapa, Bensouda amesema machafuko lazima yakomeshwe eneo hilo.

Ameonya yeyote anayechochea au kuhusika nayo kwa kutoa amri, kuhimiza au kuchangia kwa namna yoyote ile kufanya uhalifu wa kivita, anastahili kushtakiwa katika mahakama hiyo.

Bensouda aliyekuwa akizungumzia ghasia za hivi karibuni eneo hilo, alisema machafuko dhidi ya raia yanaweza kuchukuliwa kuwa uhalifu wa kivita, kwa mujibu wa Mkataba wa Roma.

Katika kauli yake nyingine iliyoonekana kuwalenga viongozi wa kundi la Hamas, Bensouda alisema kutumia uwepo wa raia kama ngao au kinga katika maeneo ya vita ya kijeshi, pia kunaweza kuchukuliwa kuwa uhalifu wa kivita.

Kwa mujibu wa Bensouda, uhalifu wowote ambao umefanywa kwa muktadha wa hali ya Palestina, unaweza kuchunguzwa na ofisi yake.

Israel inakabiliwa na maswali kuhusu kutumia risasi za moto na kuwaua Wapalestina 30 katika maandamano ya siku 10, ambayo yalikumbwa na vurugu katika mpaka wa Ukanda wa Gaza.

Januari 2015, maofisa wa Palestina walitia saini mkataba wa Roma hivyo kujiunga rasmi na ICC.

Bensouda amekuwa akiendelea na uchunguzi wa awali kubaini kama kuna ushahidi wa kutosha kuanzisha uchunguzi wa kina dhidi ya madai ya uhalifu wa kivita uliofanywa ndani ya Palestina tangu Juni 2014.

Israel imesema maandamano yanayofanyika katika Ukanda wa Gaza, ni kifumba macho tu ili vikosi vyake vishambuliwe, na ni juhudi za kuvunja uzio wa mpaka huo.

- Advertisement -

Related Articles

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Stay Connected

90,904FansLike
214,997FollowersFollow
591,000SubscribersSubscribe

Latest Articles