30 C
Dar es Salaam
Saturday, June 10, 2023

Contact us: [email protected]

MUGABE AGOMA KUKABIDHI FUNGUO RASMI ZA IKULU

HARARE, ZIMBABWE


RAIS wa zamani wa Zimbabwe, Robert Mugabe, bado anashikilia funguo rasmi za Ikulu zaidi ya miezi minne tangu alipolazimishwa kustaafu.

George Charamba ambaye ni msemaji wa Rais Emmerson Mnangwagwa, aliliambia gazeti binafsi la Standard juzi; “Kuna mtu haiambii nchi kuwa rais wa zamani bado anashikilia funguo za Ikulu.”

Kauli ya Charamba, inakuja baada ya madai kuwa laptop zilizohifadhiwa na mke wa rais huyo wa zamani, Grace Mugabe katika makontena yaliyopo Zimbabwe House, ambayo ni sehemu ya Ikulu mjini Harare, hazijulikani zilipo.

“Mnangagwa hajatia mguu Zimbabwe House wala hamiliki funguo. Inakuaje uendelee kukaa na fungua ukifahamu nyumba ina wakazi wapya?” alisema na kuhoji Charamba ambaye awali alikuwa msemaji wa Mugabe.

Mugabe (94) alilazimishwa kujiuzulu Novemba mwaka jana baada ya jeshi kuitwaa nchi kuzuia kile kilichoonekana kumrithisha madaraka mkewe Grace, ambaye alishinikiza kufukuzwa kwa Mnangagwa umakamu wa rais.

Wiki iliyopita, gazeti binafsi la Daily News liliripoti kuwa Mugabe aliyekuwa madarakani kwa miaka 37 na mkewe, wanakataa kuondoa samani na vitu vyao vingine vya thamani kutoka Ikulu.

Hata hivyo, familia haijaishi Zimbabwe House tangu walipohamia moja kwa moja katika makazi yao maarufu kama ‘Blue Roof’ kaskazini mwa Harare miaka 12 iliyopita.

Jengo la Ikulu, ambalo huonekana mara kwa mara katika televisheni, ni mahali pa mapokezi rasmi, na majengo rasmi wanayoishi viongozi yanafahamika kama Zimbabwe House.

- Advertisement -

Related Articles

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Stay Connected

90,904FansLike
213,409FollowersFollow
568,000SubscribersSubscribe

Latest Articles