25.5 C
Dar es Salaam
Thursday, December 12, 2024

Contact us: [email protected]

Ibrahim Class: Fundi umeme anayetakata kwenye masumbwi

NA GLORY MLAY 

NI dhahiri kuwa vipaji vikiibuliwa tangu utotoni na kuendelezwa vyema vijana wanakuja kuwa wazuri ukubwani na kulitangaza vyema taifa nchi za nje.

Hali hiyo inadhihirika kwa kijana Ibrahim Class ‘king Class Mawe’ ambaye anafanya vizuri katika medani za ngumi  ambazo zinamsaidia kuinua kiwango chake.

Tangu aingie katika mchezo huo ameshiriki katika mashindano mengi na kufanya vizuri na kusababisha wadau mbalimbali wa masumbwi kumtabilia kufika mbali mbali ikiwa atazingatia mazoezi.

Class jina lake lilikuwa zaidi pale alipofanikiwa kutetea ubingwa wa mkanda wa dunia wa Baraza la Ngumi Duniani (Global Boxing Council – GBC), uzito wa ‘lightweight’ baada ya kumchapa Koos Sibiya kutoka Afrika Kusini.

Pambano hilo la raundi 12, lilichezwa mwaka 2017  katika Uwanja wa Uhuru, Dar es Salaam, ambapo Class alishinda kwa pointi kutoka kwa majaji wote watatu.

KWANINI NGUMI

King Class anasema alishawishika kuingia katika mchezo huo kutokana na mapenzi aliyokuwa nayo tangu utotoni ambapo alikuwa na ndoto za kuwa mwanamasumbwi.

Anasema kuwa ndoto yake ilianza kutimia baada ya kaka yake naye anaeitwa Chaku Master kuwa mwanamasumbwi alikuwa akifanya vyema miaka kadhaa iliyopita.

“Chaku nilikuwa nikiishin naye hivyo wakati anakwenda kufanya mazoezi nilimuomba kuongozana na hali iliyonifanya kuanza kucheza licha ya kuwa ni ndoto yangu ya siku nyingi, anasema King Class.

Kocha wake wa kwanza kufundisha kucheza ngumi alikuwa ni mzee Babu Tule ambaye alimpa misingi ambayo inamfanya hadi kuwa bondia mzuri anaeshimu nidhamu na sheria za mchezo huo.

Mwaka mmoja baadaye aliamishia kwa kocha Mkongwa  Habibu Kinyogoli ambapo hapo alikutana na makocha wengi akiwemo kocha wa Kimataifa wa Mchezo wa Masumbwi nchini Rajabu Mhamila ‘Super D.

Anasema makocha hao walimpa mbinu zaidi za mchezo huo na kumjenga katika misingi thabiti ya kufikia ndoto za kifikia mafanikio.

KUSHINDA KO

Anasema mwaka 2006 baada ya kuwa chini ya kocha wa siku nyingi katika mchezo huo Kinyogoli kiwango chake kinakuwa kikiongezeka kila siku na kuwa tishio katika ngumi za amacha.

Class anasema tangu wakati huo amepambana mapambano mengi ambao alifanya vizuri na kumbukumbu yake inaonesha alifanikiwa kuwatwanga wapinzani kwa KO katika mapambano zaidi ya 10, ndicho kitu anachojivunia kwa sasa.

“Huwa najisikia faraja ninampompiga mtu kwa KO kwani inazidi  kunijengea heshima katika ngazi ya amacha ambayo ndiyo niliyopo kwa sasa ambayo nahisi sina mpinzani,” anasema Class.

SIRI YA MAFANIKIO

Anasema siri kubwa ya kufanikiwa kufanya vizuri katika mapambano yake ni kutokana na kuzingatia mazoezi, miiko, sheria na kanuni za mchezo huo ambazo kila siku huwa anaelekezwa na kocha wa Kinyogoli.

Chipukizi huyo katika masumbwi anasema kila bondia anaweza  kufanya vizuri ikiwa atajihidi kusimama imara kuzingatia yanayokatazwa katika mchezo huo.

“Moja ya vitu ambavyo avitakiwi ni uvutaji wa sigara na utumiaji wa dawa kulevya ikiwemo bangi na dawa nyingine ambazo ufanya kuwa na uhamuzi usio sahihi,” anasema Class.

UFUNDI UMEME

Class anasema  licha ya kujihusisha na masumbwi pia ni fundi wa vifaa vya umeme ikiwemo pasi, televisheni, friji,specer na vifaa vingine vinavyotumia umeme.

“Kipindi ambacho ninakuwa nyumbani sina pambano lolote huwa ninafany kazi umeme watu wananiletea vitu vyao kama pasi, televisheni na vingine vingi,” anasema. 

VIFAA VYA MICHEZO

Anasema ili kuundeleza mchezo  ni bora vifaa vikatolewa bure au kwa bei nafuu kwenye klabu mbalimbali zinazoinua mchezo huu kwa vijana wadogo ambao mara wamekuwa wakitatizwa na nyenzo za kufanyia mazoezi.

“Ukiangalia vijana chipukizi wapo wengi lakini kitu kinachiwa kwamisha ni vifaa vya michezo, wadau na Serikali inatakiwa kuwa na utamaduni wa kutoa vifaa kila mwaka kwa vijana hawa wanaopenda kujifunza.

“Au wangekunguza maana vifaa vinauzwa bei kubwa madukani hivyo vijana wengi wanashinda kumudu gharama hizo hivyo vioaji vyao vinakuwa vinapotelea hewani,” alisema.

AWASHAURI MABONDIA

Class anasema ikiwa bondia atatumia Sigara au akivuta bangi ufanisi wake unakuwa mdogo kutokana na kifua kuwa kizito na kushindwa kumaliza raundi za mchezo au anaweza kupigwa kwa KO.

Hivyo anawashauri mabondia ambao wanajihusisha utumiaji wa tumbaku kuhachana na tabia hiyo ili kufikia malengo waliojiwekea katika masumbwi.

Pia anasema unywaji wa pombe nayo ni sehemu inayonyong’onyesha viungo, ikiwa bondia atahitaji kufanya vizuri ni vyema akaepiuka utumiaji wa pombe.

Kingine anasema kuwa suala la uzinzi nalo ni tatizo kwa baadhi ya wanasumbwi na ndiyo sababu kubwa inayowafanya kushindwa kufanya vyema ulingoni na kuambulia kupigo kikali.

Hivyo anawaomba wanamasumbwi chipukizi na wakongwe kujiepusha na hanasa hizo ambayo zinarudisha nyuma harakati za maendeleo ya mchezo huo nchini.

- Advertisement -

Related Articles

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Stay Connected

90,904FansLike
214,997FollowersFollow
592,000SubscribersSubscribe

Latest Articles