23.2 C
Dar es Salaam
Saturday, July 27, 2024

Contact us: [email protected]

Hukumu dhidi ya Mbowe Julai 17

mboweNA RODRICK MUSHI, HAI

HUKUMU ya kesi ya kumshambulia mwangalizi wa ndani wa uchaguzi mkuu wa mwaka 2010 inayomkabili Mbunge wa Jimbo la Hai, Freeman Mbowe, iliyotarajiwa kutolewa jana katika mahakama ya Wilaya ya Hai, imeahirishwa hadi Julai 17 mwaka huu baada Mbowe kushindwa kufika mahakamani.

Mbowe ambaye pia ni Mwenyekiti wa Chama cha Demokrasia na Maendeleo (Chadema),ilidaiwa alishindwa kufika mahakamani n kutokana na kutoa udhuru wa kubanwa na kazi za serikali likiwamo bunge la bajeti linaloendelea Dodoma.

Hukumu ya kesi hiyo imeahirishwa kwa mara ya pili sasa. Kwa mara ya kwanza hukumu ilikuwa itolewe Mei 11 mwaka huu lakini ilishindikana baada ya Hakimu Mfawidhi, Denis Mpelembwa kuwa
nje ya mahakama kwa shughuli za ofisi.

Akiahirisha kesi hiyo, Hakimu Mkazi Mfawidhi Mpelembwa alisema alishindwa kufika mahakamani hapo kutokana na kubanwa na shughuli za serikali hivyo kupangiwa siku nyingine kwa ajili ya kusomewa
hukumu.

Katika kesi hiyo ya jinai namba 73 ya mwaka 2011, Mbowe akiwa mmoja kati ya wagombea ubunge wa Hai, mwaka 2010, anadaiwa kumshambulia Nassir Yamin katika Kijiji cha Nshara, Kata ya Machame Kaskazini, Wilaya ya Hai mkoani Kilimanjaro.

Katika uchaguzi huo wa mwaka 2010, Mbowe alishinda kwa kupata kura 28,585 akifuatiwa na Fuya Kimbita (CCM) aliyepata kura 23,349, Hawa
Kihogo (UDP) kura 258 na Petro Kisimbo (TLP) 135.

- Advertisement -

Related Articles

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Stay Connected

90,904FansLike
214,997FollowersFollow
589,000SubscribersSubscribe

Latest Articles