25 C
Dar es Salaam
Tuesday, December 17, 2024

Contact us: [email protected]

Huduma za Malaria sasa kutolewa bure nchi nzima

*Serikali yasema lengo ni kutokomeza ugonjwa huo sugu

*Yawaonya wanaotumia nyandarua kufugia kuku, bustani

Na Esther Mnyika, Mtanzania Digital

WAZIRI Mkuu Kasimu Majaliwa amesema katika mchakato wa kutokomeza Malaria Watanzani wote watapata huduma ya kutibu malaria bure katika vituo vyote vya afya nchini.

Akizungumza leo Aprili 25, jijini Da es Salaam katika maadhimisho ya Kitaifa ya siku ya malaria duniani na wadau mbalimbali yaliyofanyika katika viwanja vya Mnazi Mmoja, Majaliwa amesema bado inahitajika nguvu katika kutokomeza ugonjwa huo ifikapo mwaka 2030.

“Kutokana na kutoa wito wa kupunguza malaria wananchi watapata huduma bure kupimwa malaria, sindano kali ya malaria bure, dawa ya malaria bure, dawa ya Asp bure na kutolewa bure katika vituo vya afya,” amesema Majaliwa.

Aidha, Majaliwa ambaye alimuwakilisha Rais Dk.Samia Suluhu Hassan ametoa agizo kwa Serikali za Mitaa kuanzia sasa kuwa ni marufuku kutumia chandarua chenye dawa kwa ajili ya malaria kuweka kwenye bustani za mboga.

Amesema licha ya maambukizi malaria kupungua bado vifo vinaendelea kutokea vinavyosababishwa na ungonjwa huo, ambapo takwimu zinaonyesha mwaka 2015 ilikuwa asilimia 14.8 hadi sasa umepungua hadi asilimia 8.1 huku akitaja mikoa kinara.

“Mikoa inayoongoza kwa maambukizi dhidi ya malaria ni Tabora asilimia 23, Mtwara asilimia 20, Kagera asilimia 18, Shinyanga asilimia 16 na Mara asilimia 15, tunahitaji kutokomeza malaria tunapoteza nguvu kazi ya Taifa,” amesema Majaliwa.

Ameipongeza mikoa yote tisa ambayo imeweza kutokomeza malaria ikiwemo Dar es Salaam, Iringa, Arusha, Songwe, Njombe, Manyara,Singida na mingineyo.

Wakati huo huo Waziri Mkuu Majaliwa amezindu Baraza la Malaria la Kitaifa lenye lengo la kuwawekea mipango ambayo itawafikia wananchi kudhibiti malaria.

Alisema baraza hilo limeundwa na wajumbe mbalimbali ambalo litashirikiana Serikali, Taasisi mbalimbali na wadau ili kuleta mafanikio yatakayotona na juhudi zao.

“Kauli mbiu ya mwaka huu ni wakati wakutokomeza malaria ni sasa badilika, wekeza, tekeza na Zero malaria inaanza na mimi kaulimbiu nimeipenda,” amesisitiza Mjaliwa.

Naye Waziri wa Afya Ummy Mwalimu alisema asilimia 94 ya watanzania wapo hatarini kupata ugonjwa wa malaria na tunashudia vifo vinavyotokana na malaria ugonjwa huo bado ni tishio.

Amesema takwimu zinaonyesha maambukizi ya malaria nchini yamepungua kwa asilimia 50.

“Uhaba wa rasmali kwa ajili ya kutelekeza mpango mkakati wa malaria mwaka 2021 hadi 2025 ni asilimia 57,” amesema Ummy.

Naye Kaimu Mkurugenzi wa Kuratibu na Kukuza Utafiti (NIMR), Dk. George Praygod amesema wamepunguza vifo vya maralia kwenye miaka ya 2000 walikuwa na wagonjwa zaidi ya laki moja sasa wana vifo chini ya elfu kumi ambayo ni mafanikio.

“Mradi wa MSMT unaleta mabadiliko makubwa sana unaweza Kufanya utafiti
Utaleta taarifa muhumi kwa wizara ya afya kusaidia serikali kupambana na malaria. Tumemsikia Waziri Mkuu taasisi za utafiti ziendelee kutumika katika utafiti,”alisame Dk,. Praygod.

- Advertisement -

Related Articles

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Stay Connected

90,904FansLike
214,997FollowersFollow
592,000SubscribersSubscribe

Latest Articles