26.1 C
Dar es Salaam
Sunday, November 17, 2024

Contact us: [email protected]

Hotuba ya Joseph Kabila itakayobaki kwenye kumbukumbu DRC

ALHAMISI ya wiki iliyopita, Jamhuri ya Kidemokrasia ya Kongo (DRC), ilishuhudia uhamishaji wa madaraka wa kwanza wa kihistoria kutoka Rais aliyechaguliwa kidemokrasia kwenda kwa mrithi wake aliyepitia njia kama hiyo.

Si hivyo tu, bali ni uhamishaji madaraka kati ya Rais anayeondoka kutoka chama kwenda kwa rais mpya wa chama cha upinzani.

Hata hivyo, kusudio la safu makala haya linalenga kuitoa hotuba aliyeitoa rais anayeondoka kama ilivyotafsiriwa na Mwandishi Wetu.

Ni hotuba ya kijasili na dhamira, ambayo mkuu wa nchi aliyemaliza muda wake, Joseph Kabila Kabange, aliitoa kuwaaga watu wa Kong. Endelea…

Miaka 18 iliyopita katika siku, ambayo tumeikaribia, kwa  neema ya Aliye Juu, na kufuatia mchanganyiko wa mambo ya bahati mbaya, nikawa hakimu mkuu katika mazingira, ambayo yalikuwa na changamoto nyingi kubwa na mbaya.

Na kwa uwapo wa sintofahamu kuhusu hatima ya nchi yetu kama taifa… kukwama kwa uchumi, mfumuko wa bei unaopaa kwa kasi na deni la nje lisilohimilivu na kuandamwa na migogoro ya kivita yenye madhara makubwa na kugawanyika kwa nchi katika himaya nyingi mno kutokana na uwapo wa mabwana vita wanaoziendesha, Jamhuri ya Kidemokrasia ya Kongo, nchi yetu, kwa kweli ilikuwa inachungulia shimoni.

Tiba ya mshtuko ilikuwa ikihitajika haraka kuzuia Taifa kuingia shimoni na kutengeneza mazingira ya kurudisha afya.

Kana kwamba hayo hayakutosha, Mzee Laurent-Désiré Kabila aliyeacha kumbukumbu adhimu, ambayo iliibua matumaini makubwa miongoni mwa watu wa Kongo walioteseka na miongo mingi ya udikteta na usimamizi mbaya aliuawa na nguvu za uovu, hata kabla ya misingi ambayo ndiyo alikuwa ameiweka, ambayo wana na mabinti wa Kongo wangejivunia haijahalalishwa.


Kulikuwa na ulazima wa kuepuka kutoweka kwa ndoto hizo kutokana na kifo chake hicho. Ni kwa unyenyekevu uliotokana na mwamko wa ukubwa wa kazi lakini pia kwa dhamira ya kufanikiwa, ambayo hutokana na imani kubwa katika Mungu na watu wake kwamba katika siku, ambayo jua lilikuwa likiwaka ya Januari 26, 2001, nilijibu wito wa taifa kwa kuchukua kiapo kwa mara ya kwanza, kiapo cha kikatiba kama Rais wa Jamhuri hii.

Tangu wakati huo, tumefanya mengi, hatuwezi kujidai tulifanya kila kitu. 
Kwa kweli, licha ya maovu na matendo mabaya ya maadui wa watu wetu, sijawahi kamwe kusaliti kiapo changu, wala dhamira yangu haijawahi kudhoofishwa na kwa msaada wenu, hakika vikwazo vingi tumevishinda, kutokana na mambo mazuri yaliyofanyika. Kwa kutazama pale tulipokuwa miaka 15 au zaidi iliyopita, kuna kitu cha kusherehekea,

Hivyo, shukrani kwa uhamasishaji madhubuti wa watu wetu wote hadi katika mazungumzo ya kudumu na wadau wakuu wa kisiasa na kijamii kama njia ya kuzuia migogoro na kusuluhisha mizozo, hadi matendo ya mashujaa wetu jasiri wa ulinzi. Kila siku ipitayo, diplomasia iliyoandaliwa vyema, iliyo hai, yenye utaalamu na ufanisi, mageuzi ya aina yake ya kitaassi pamoja na utawanyaji madaraka majimboni na marekebisho ya karibuni ya kanuni ya madini na sera madhubuti za fedha na usimamizi wa fedha za umma, nchi imesuluhishwa na kuunganishwa, uchumi umetulia na kuimarika, ujenzi upya umeshuhudiwa, upatikanaji wa huduma za msingi za kijamii umeboreshwa na maendeleo ya kuridhisha yameshuhudiwa katika masuala ikiwamo demokrasia na uanzishwaji wa utawala wa sheria, ikiwa ni pamoja na uendeshaji wa mara kwa mara wa chaguzi huru na za kidemokrasia.

Mgogoro wa uwaniaji madaraka mwaka 1960, ukifuatiwa na mauaji ya Januari 1961 ya shujaa wetu wa Taifa, Patrice Emery Lumumba uliweza kutatuliwa shukrani kwa hatua tulizochukua na chini ya uongozi wetu kwamba madaraka yarudishwe kwa watu wa Kongo, ambako ndiko iliko dhamana yake asilia.

 Ndugu wazalendo wenzangu wapendwa, Desemba 30 mwaka jana, kwa mara ya tatu mfululizo, mlienda kupiga kura kumchagua Rais wa Jamhuri na manaibu wa Taifa, na kwa mara ya pili, kuchagua wawakilishi wenu katika mabunge ya majimbo yenu.

Asanteni kwa ukomavu wenu, chaguzi zilifanyika kwa utulivu, kitu ninachowapongeza. Na kwa mara ya kwanza kwa ukubwa wao, kama nilivyoahidi mchakato mzima wa uchaguzi uligharimiwa na Serikali ya Jamhuri ya Kongo.

Uhuru wa kujiamulia mambo wa taifa, uhuru kamili wa taifa letu na heshima ya watu wetu ni wa thamani sana. Imeshuhudiwa kuwa ni kwa sababu halisi inayoleta hali ya kujivunia. Inapaswa kuendelea kulindwa na kuendelezwa, kwa kadiri ya utajiri wa utamaduni wetu mtambuka.

Kanuni na heshima hii ni msingi wa taifa letu, na kichocheo cha kuishi pamoja. Kama ambavyo mababa zetu waasisi na watangulizi wetu walivyotuachia, ndivyo nami ninavyoikabidhi kwa mrithi wangu. Ni kwa ajili ya hatima ya nchi yetu na uhai wa watu wetu. Mengine mengi zaidi ambayo hayakuandikwa katika historia ya nchi yetu, ambayo yanaifanya kuwa mwasisi katika eneo hilo katika eneo la kusini mwa Sahara la katikati mwa Afrika.

Chaguzi za Desemba 30 kama nilivyoahidi zimesafisha njia ya uhamishaji wa madaraka ya kiraia kwa amani na iliyostaarabika kati ya mkuu wa nchi anayeondoka na mkuu wa nchi aliyechaguliwa, kitu ambacho ni ndoto iliyotimia.

Zaidi ya hayo, kamali iliyoshinda. Hii pia ni dalili ya kung’ara kwa utamaduni wa demokrasia katika nchi yetu kwamba mwenye bahati ya kuchaguliwa, naam, mnufaika wa mabadiliko haya ya kihistoria katika kiti cha juu kabisa cha uongozi wa taifa letu, anatokea upinzani!.

Hapa ndipo mahali ninapopata fursa ya kusisitiza kwa niaba yenu na yangu mwenyewe pongezi zetu za dhati na kumtakia mafanikio Rais aliyechaguliwa, Félix Antoine Tshisekedi Tshilombo.

Kwamba namhakikishia ushirikiano na wakati wowote na atakaponihitaji na kwa maslahi mapana ya nchi yetu.

Nalisema hili kwa nguvu zaidi kwamba chaguo lililofanywa na watu halijaoanisha wingi wa kura za urais na zile za wabunge, nawahimiza viongozi wa kisiasa kuishi katika mwelekeo mmoja, kuungananisha juhudi zao na kufanya kazi pamoja ili kukidhi mahitaji ya watu na ustawi wa taifa…

- Advertisement -

Related Articles

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Stay Connected

90,904FansLike
214,997FollowersFollow
591,000SubscribersSubscribe

Latest Articles