29.2 C
Dar es Salaam
Saturday, November 16, 2024

Contact us: [email protected]

HOSPITALI YAKOSA MAJOKOFU YA KUHIFADHI MAITI

 

Na GURIAN ADOLF- SUMBAWANGA

 

MAJOKOFU ya chumba cha kuhifadhi maiti katika Hospitali ya Mkoa wa Rukwa, yameharibika kwa zaidi ya mwezi mmoja sasa na kusababisha usumbufu mkubwa kwa jamii.

Kuharibika huko kumeongeza gharama kwa baadhi ya ndugu wa marehemu ambao wanapenda kuhifadhi miili ya marehemu wakati wakiwasubiri ndugu wengine walioko mbali kabla ya maziko.

 

Mmoja wa wakazi wa Mji wa Sumbawanga, Maria Kayanda ambaye mjomba wake alifariki dunia juzi, alisema walilazimika kufanya maziko haraka kutokana na kukosa mahali pa kuhifadhi mwili wa ndugu yao.

 

Mmoja wa wafanyakazi wa chumba cha kuhifadhi maiti katika hospitali hiyo ambaye hakutaka jina lake litajwe gazetini, alikiri kuharibika kwa majokofu hayo kwa muda wa zaidi ya mwezi mmoja sasa.

 

Alisema uongozi wa hospitali hiyo ulileta mafundi na wakatengeneza lakini siku chache baadaye yaliharibika.

 

Kaimu Mganga Mkuu wa Hospitali ya Mkoa wa Rukwa, Emanuel Matika, alikiri kuharibika kwa majokofu hayo ambapo alisema wamekwishatoa  taarifa kwa Wakala wa Huduma za Ufundi na Umeme (Temesa).

Hata hivyo, Dk. Matika alisema tatizo ni ukosefu wa fedha kutokana na utaratibu wa Temesa kuwa ni lazima walipwe fedha kwanza ndipo wafanye matengenezo ya majokofu hayo. Hata hivyo, alisema mchakato wa kutafuta fedha unaendelea.

Dk. Mtika alisema: “Kipindi hiki tunatumia dawa ya fomalini kuzuia miili isiharibike haraka kabla ya kusafirishwa na ndugu kwenda kuzika,” alisema Dk. Matika.

- Advertisement -

Related Articles

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Stay Connected

90,904FansLike
214,997FollowersFollow
591,000SubscribersSubscribe

Latest Articles