20.5 C
Dar es Salaam
Saturday, August 20, 2022

WANAVIJIJI WATAKA WANASIASA KUTEKELEZA WALIYOYAAHIDI

Na ELIUD NGONDO – SONGWE

WANANCHI wa Vijiji vya Ndalambo na Mengo, Kata ya Ndalambo wilayani Momba mkoani Songwe, wamewataka wanasiasa kutekeleza kile walichoahidi kwenye kampeni zao.

 

Wananchi hao wameeleza msimamo huo jana mbele ya Mwenyekiti wa Chama Cha Mapinduzi (CCM) Wilaya ya Momba, Twaha Masoud, kwenye mkutano wa hadhara wa kumtambulisha mgombea udiwani wa CCM, Flavian Sichizya.

 

Walisema wanayo kero kubwa na ya siku nyingi ya kupata maji safi na salama ingawa waliahidiwa kutatuliwa kero hizo na wanasiasa, huku wakisisitiza kuwa hadi sasa hakuna ahadi yoyote iliyotekelezwa na viongozi waliopo madarakani.

 

Osea Mgala, mkazi wa Kijiji cha Ndalambo, alisema wanakatishwa tamaa na viongozi ambao hawatekelezi ahadi zao kama ambavyo waliahidi wakati wakitafuta madaraka ya kutawala.

 

“Wanasiasa walitoa kauli ya kuaminiwa lakini hadi sasa hakuna hata dalili ambazo zinaonyesha kutekelezwa kwa ahadi hizo, tunaendelea na shida zetu za kukosa maji safi na salama ambacho ndicho kilio chetu,” alisema.

Godfrey Mwanguku alisema katika vijiji

hivyo wameshindwa hata kufanya shughuli za maendeleo kutokana na shida ya upatikanaji wa maji.

Akijibu hoja hizo, Masoud alisema wananchi wanatakiwa kuwaamini viongozi wanaotumia Katiba ya chama kuahidi na si wanaotumia majukwaa pekee.

Alisema mwanasiasa akitumia katiba ya chama ni rahisi kutekelezwa ahadi alizoziahidi kutokana na utaratibu ulivyo, lakini wale wanasiasa ambao huongea majukwaani bila kuwa na Katiba ni waongo.

“Ukitoa ahadi kwa wananchi kwa kuongozwa na katiba ya chama chako lazima utaitekeleza tu, kwani sheria itakubana lakini kama hakuna

katiba yoyote ni rahisi kudanganywa na kutochukuliwa hatua yoyote,” alisema Masoud.

 

“Wananchi wanatakiwa kuiamini CCM kutokana na kuongea mambo ambayo yameandikwa ndani ya Katiba yake, hivyo kuna baadhi ya vyama havina hata katiba hali ambayo wananchi hawawezi kuvibana,” alisema Masoud.

- Advertisement -

Related Articles

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Stay Connected

90,904FansLike
199,058FollowersFollow
551,000SubscribersSubscribe

Latest Articles