NA ARODIA PETERDODOMA
MBUNGE wa Muleba Kusini, Profesa Anna Tibaijuka (CCM), ameishauri Serikali kuimarisha ushirikiano wa sekta binafsi katika utoaji wa huduma za afya nchini.
Profesa Tibaijuka alisema hayo jana bungeni wakati akichangia hotuba ya Wizara ya Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto bungeni.
“Utaratibu wa Public Private Partnership ni muhimu, naomba uendelee, tunapoboresha hospitali za Serikali tusisahau umuhimu wa kuhakikisha kwamba zile ambazo tulikuwa nazo tunalinda uwezo wake.
“Sina budi kusema kwamba hospitali siyo majengo ila ni huduma na katika hili, Waziri pia aangalie hali halisi ya hospitali za rufaa, napongeza juhudi za Serikali ya awamu ya nne iliyokamilisha Hospitali ya Mloganzila lakini hospitali hiyo ni hospitali majengo kwani hakuna hospital town pale kwa ajili ya madaktari kukaa karibu na hospitali”alisisitiza Profesa Tibaijuka.
“Hivi kama kuna dharura pale daktari anafikaje Mloganzila? Kwa hiyo naona kuna haja ya kufanya uwekezaji kukakikisha kwamba kituo kinafanya kazi.
Akizungumzia Hospitali teule ya wilaya ya Muleba ya Rubya mbunge huyo alimuomba Waziri Ummy kupeleka mashine ya kupima wingi wa virusi vya Ukimwa (vairolod) ambapo alisem a wamesikia mashine hiyo ililetwa hospitalini hapo lakini imehamishwa na kupelekwa Hospitali ya Bukoba.
“Mheshimiwa Spika licha ya upungufu wa vifaa tuna uhaba wa watumishi wa maabara, hivi tunavyozungumza hospitali ya Rubya haina any degree order kwenye famasi na hii ni hospitali inayohudumia wakazi 700,000, kama una idadi hiyo ya wananchi huna maabaara ambayo ina equalified technition unaona kwamba hapo huwezi kutoa huduma inayostahiki”alisisitiza mbunge huyo.
Mbunge wa Viti Maalum Mkoa wa Tanga, Sonia Magogo (CUF) alisema tatizo ni elimu duni juu ya matatizo ya udumavu na utapiamlo.
Mbali na hilo mbunge huyo aliiomba Serikali iangalie uwezekano wa kutoa elimu na kufanya utafiti kwa jamii juu ya matatizo mbalimbali ya kiafya yanayojitokeza mara kwa mara.
Alisema katika siku za karibuni, jamii inakabiliwa na tatizo la wanawake kutoshika mimba, mimba kutungwa nje ya kizazi, watoto wachanga kufariki dunia na upungufu wa nguvu za kiume.
Mbunge wa Viti Maalum, Suzan Lyimo (Chadema) alisema hospitalini karibu zote za rufaa hazina mashine za mionzi ya kutibu ugonjwa wa jambo ambalo linachangia vifo vingi kwa Watanzania.
“Hakuna haja ya kupandisha hadhi hospitali bila kuwepa vifaa, mimi ni mjumbe wa Kamati ya Maendeleo ya Jamii, huko tulikotembelea wakuu wa hospitali kilio chao kikuu ni kununua mashine na wagonjwa kutoka kanda zote wanalazimika kwenda Hospitali ya kansa Ocean road Dar es Salaam.