24.2 C
Dar es Salaam
Tuesday, April 16, 2024

Contact us: [email protected]

Historia yaandikwa Katiba Mpya

Samuel Sitta
Samuel Sitta

NA NORA DAMIAN, DAR ES SALAAM

HISTORIA mpya imeandikwa Tanzania baada ya Mwenyekiti wa Bunge Maalumu la Katiba, Samuel Sitta, kukabidhi Katiba inayopendekezwa kwa Rais Jakaya Kikwete na Rais wa Zanzibar, Dk. Ali Mohamed Shein mjini Dodoma.

Makabidhiano hayo yalifanyika jana mjini Dodoma, katika sherehe zilizoanza saa 8 mchana yakitanguliwa na burudani kutoka vikundi mbalimbali huku wajumbe wanawake wa Bunge Maalumu la Katiba wakiwa katika sare maalumu ya vitenge maarufu vya Makenzi.

Viongozi mbalimbali walihudhuria sherehe hiyo wakiwamo mabalozi wanaoziwakilisha nchi zao, viongozi wa dini, vyama vya siasa, wasanii na wananchi.

Akizungumza katika sherehe hizo, mwakilishi kutoka Zanzibar, ambaye pia ni Mbunge wa Wawi, Hamad Rashid Mohamed (CUF), alisema wakiwa ndani ya Bunge la Katiba walihakikisha wanaziondoa kero za Muungano bila kuathiri muundo ulioasisiwa na waasisi wake.

“Nataka kipekee niwapongeze wajumbe kutoka Zanzibar kwa kuwa kama kuna wakati walikuwa na mimba na hawajui watazaa lini, ni pale walipokuwa wanatafuta theluthi mbili kwa upande wa Zanzibar, lakini nashukuru Wazanzibari walifanya kazi usiku na mchana kuhakikisha inapatikana.

“Hakuna sababu tena ya kutounga mkono mfumo wa Serikali mbili ambao unavua makoti ya Muungano. Zanzibar sasa inaweza kukopa hata pale ambapo hakuna masharti ya aina yoyote, inaweza kukopa bila hata kuwapo kwa idhini ya Serikali ya Jamhuri ya Muungano,” alisema.

- Advertisement -

Related Articles

1 COMMENT

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Stay Connected

90,904FansLike
214,997FollowersFollow
586,000SubscribersSubscribe

Latest Articles