Na Mwandishi Wetu, Mtanzania Digital
Mfuko wa kusaidia biashara ya ubunifu Afrika Mashariki wa HEVA (EACBF) umetoa fursa kwa wabunifu kuomba mkopo utakaowawezesha kuwavusha baada ya kupitia kipindi cha janga la Corona.
Utaratibu huo umewekwa kuanzia mwaka huu, 2021 na kuendelea kwa waombaji waliofanikiwa, kupitia uwekezaji wa madeni wa kati ya dola za Kimarekani 20,000 na 50,000, kwa kipindi cha zaidi ya miaka minne.
Tayari HEVA wametangaza kupokea maombi ya waombaji 76 wenye sifa katika jumla ya maombi 430 kutoka Kenya (248), Uganda (59), Ethiopia (33), Tanzania (30) na Rwanda (60).Maombi yote yaliwasilishwa kati ya Septemba na Oktoba 2020, pindi maombi ya EACBF yalipofunguliwa rasmi.
Waombaji 76 kati ya 430 wana sifa za kupewa fedha, wakiwa wamefikia mahitaji yote kama biashara yenye kipato kisichozidi dola 20,000, na mwajiriwa/mfanyakazi takriban mmoja (kama kazi ya ziada ama kazi ya muda wote).
Waombaji wote wenye sifa wamesajiliwa na wanafanya kazi kwenye nchi za Afrika Mashariki kama ifuatavyo: Kenya (40), Uganda (11), Ethiopia (4), Tanzania (7) na Rwanda (14).
Katika makampuni hayo, 28 ni makampuni yanayoendeshwa na wanawake, wakati 43 yanamilikiwa au kuendeshwa na wanaume, wengine watano hawakupenda kuelezea jinsia zao.
Ugawaji wa mnyororo wa thamani ulikuwa kama ifuatavyo: Ufundi (3),Elimu ya Utamaduni (4), Miundombinu ya Kitamaduni (3), Utalii wa Kitamaduni (4), Vyombo vya Habari vya Kidijitali (10), Matukio (1), Mitindo (21), Filamu na Upigaji Picha (9), Chakula (7), Upambaji wa ndani (3), Muziki wa Live (4), Utayarishaji wa Muziki (6) na Utengezaji/Ususi wa nywele na Urembo (1).
Waombaji waliofanikiwa watapitia hatua kadhaa: jopo la biashara kuangalia uwezekanaji wa biashara hizi; jopo la ubunifu ambalo litaangalia bidhaa kama zina soko; na kisha jopo la mawasilisho ambalo litahoji biashara kwa kina kueleza vizuri mfungamano na vigezo vya fungu hilo.
Biashara hizi zitapitia mchakato wa ukaguzi kuangalia ukubalifu wao, na kisha kupitia hatua ya ukaguzi wa hesabu za matumizi na mapato kutathimini uwezo wa biashara kwendana na kiasi cha mkopo kilichoombwa.
Mfuko wa kusaidia biashara ya ubunifu Afrika Mashariki una thamani ya dola za Kimarekani 380,000, ni nyongeza ya ufadhili uliopo wa HEVA, yaani Growth Fund, ulioundwa kutoa ukuaji wa mitaji kwa biashara za size ya kati katika sekta ya ubunifu nchini Kenya, na sasa Afrika Mashariki kwa miaka michache ijayo.
Mfuko huo unatoa ufadhili kwa biashara za ubunifu kusaidia kujenga tena minyororo ya thamani iliyokatishwa kutokana na mlipuko wa COVID-19, pamoja na, kuongeza uwezo wa uzalishaji, kupanua misaada, kuongeza mgawanyo wa soko, kuongeza muingiliano wa minyororo ya thamani nyumbani na katika kanda; kusaidia uhamaji wa kuelekea uuzaji usiohitaji uwepo wa mtu (low-touch) na uwezakano wa kijiditali; na kuzifanyia kazi fursa mpya.
Wakiuru Njuguna ambaye ni Mshirika na Meneja wa Uwekezaji wa HEVA amesema: “HEVA imejipa sharti kutoa mtaji katika sekta ya ubunifu na tunafurahi hasa kuhusu kuweza kutanuka Afrika Mashariki yote hususan katika nyakati kama hizi ambazo upatikanaji wa mtaji ni mfinyu.
“Tuna uelewa juu ya changamoto fulani fulani ambazo biashara kwenye sekta hii zinakumbana nazo na matokeo yake, tuna matumaini kuwa matokeo ya uwezashaji huu utakuwa ni ushuhuda wa utoaji zaidi wa mitaji katika biashara za Afrika Mashariki kwenye sekta ya ubunifu.
“Lengo letu ni kutoa mitaji zaidi kwakuwa tunatazamia kukusanya dola milioni 20 kwa sekta ya kanda katika miaka mitatu ijayo,” amesema.